NANI ANAYEFANYA MAAGIZO KATIKA MAISHA YAKO?

David Wilkerson (1931-2011)

"Tukiishi kwa roho, na tuenene kwa Roho" (Wagalatia 5:25). Mtume Paulo anatupa maagizo haya rahisi sana kwa maneno wazi, "Ikiwa Roho Mtakatifu anaishi ndani yenu, aca awe na udhibiti kamili wa maisha yako."

Sisi sote tunaongozwa na Roho. Alitumwa kuwa muda wetu wa daima, asio kuwa na makosa, na anaishi katika wote wanaokiri Kristo kama Bwana na Mwokozi. Wakristo wengi hawana shida kukubali kwamba Roho Mtakatifu anatuongoza kwa Yesu, na hatuna shida kuamini kwamba Roho anaendelea kufanya kazi ndani yetu wakati wote.

Tunatowa heshimu kwa Roho, tunahubiri juu yake, tunafundisha juu ya zawadi na matunda yake, na wengi wetu tumemwomba kwa ajili ya faraja wakati wa mgogoro. Tunamwomba, tunamtafuta, kumwomba aifanye mbingu na kufufua kanisa lake, na kupata udhihirisho halisi wa kuishi kwake. Lakini inaonekana kwamba tunajua kidogo sana juu ya maana ya kutembea ndani ya Roho.

Kuelewa ukweli juu ya kutembea ndani ya Roho inaweza kuwokoa wengi kutoka kwenye kuchanganyikiwa, ugomvi, dhiki, kutokujali, hata tamaa za mwili. Kwa hiyo, ukweli huu ni nini? Paulo ameielezea wazi wazi kwakifupi: Kutowa mapenzi yako kwa Roho Mtakatifu na uamini ukimya wake, sauti ndogo kukuongoza katika vitu vyote. Kwa kweli, Neno la Mungu linasema, "Hatua za mtu mwema zaimalishwa na Bwana" (Zaburi 37:23). Na ni nani anayefanya maagizo? Roho Mtakatifu!

Mwili una mapenzi yake yenye ukaidi na hufanya kama unavyotaka. Unafanya chochote unachochagua na kisha kumwomba Mungu abariki chaguzi hizo zote, ukisema, "Mungu unipe akili nzuri ili niweze kufanya maamuzi ya akili. Mimi siwezi kumngojea ili aniongoze. "Lakini hata Kristo mwenyewe alisema, "Mimi sewezi kufanya neno mwenyewe ... kwa sababu siyatafuti mapenzi Yangu mimi, bali mapenzi ya Baba aliyenituma" (Yohana 5:30). Kama Yesu alivyomngojea Baba, daima alikuwa anatafuta akili zake, tunapaswa kufuata mfano wake mzuri.