MUSUKUMO KWA AJILI YA KRISTO

David Wilkerson (1931-2011)

Katika kuzingatia suala la kuongeza uwamuzi wetu kwa ajili ya Kristo, ni lazima tuangalie mafundisho ya Kristo juu ya unyenyekevu. "Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atayejijidhili, atakwezwa" (Mathayo 23:12). Yesu hapa alikua anawaita Mafarisayo kwa tabia zao zaa kiburi (23:5-7). Wanajua Maandiko na wanaweza kutafsiri Neno kwa raia, lakini maisha yao hayana kipimo.

Ikiwa sisi ni waaminifu mbele ya Mungu, hata wenye bidii kati yetu wanapaswa kukubali dhambi zinazohusiana nao. Kwa mfano, mtu anapenda kutambuliwa. Wakati Yesu aliwaraumu Mafarisayo, alikuwa akisema, "Mnataka uangalizi. Mnataka viti vyema katika mikutano ya umma na kupenda kutambuliwa mitaani." Walikuwa na kiburi na kujisifu, wakiwa na ukosefu wa kunyenyekea kabisa.

Katika msingi wake, unyenyekevu ni utegemezi wa jumla kwa Bwana. Neno "utegemezi" linamaanisha "kuamini kwa vitu vyote, katika vitu vyote." Uaminifu wa kweli hauacha kusema, "Mimi ni dhaifu," lakini pia husema, "Yeye ni mwenye nguvu." Na imani hiyo ya kutegemea inahitaji unyenyekevu.

Yesu ni mfano wetu wa unyenyekevu. Bwana aliyeumba vitu vyote na ambaye vitu vyote viliumbwa, alitegemea kabisa Baba yake. Alisema mara kwa mara, "Sifanyi neno kwa nafsi yangu . . . kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo" (Yohana 8:28-29).

Ikiwa unataka musukumo kwa ajili ya Yesu, omba Roho Mtakatifu aingie ndani katika moyo wako na akuoneshe tamaa yoyote ya kujisifu. Yesu anasema, "Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atayejijidhili, atakwezwa" (Mathayo 23:12).