MUNGU HUFURAHIYA WA TOTO WAKE

David Wilkerson (1931-2011)

Hapa ni silaha yenye nguvu kwa kila mfuasi wa Yesu: Lia! Lia sana kwa moyo wako wote kama Daudi alivyofanya (angalia Zaburi 34:6). Nenda kwa Bwana na ukiri dhambi yako na kujitokezea mbele ya mapenzi yake, ukisema, "Bwana, najua unanipenda na uko tayari kunisamehe, natubu mbele yako hivi sasa."

Kwa wakati huu unakiri, wewe hauna tatizo na Mungu tene. Ni bure kufikiri unaweza kulipa kiasi chochote kwa dhambi yako. Mungu anakupenda sana kiasi kwamba akamtoa Mwanawe, Yesu, ambaye tayari amefanya malipo yote. Msaidizi wako mwenye rehema na upendo ana hamu ya kukusaidia na kukupa: "Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Nakama mtu akitenda hdambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki" (1 Yohana 2:1).

Strolling akitembea sambamba pamoja na mjukuu wangu mdogo, Tiffany, akipitia ukuta wa chini wa saruji. Nilimchukua kutoka nyuma ili kumzuia kuanguka, lakini alijaribu kujitoa mikononi mwangu. Hatimaye nirimuachilia aende, naye akaenda zaidi, ingawa bila kujijeruhi mwenyewe. Alipoanguka, sikumuacha mwenyewe, bila shaka. Sikusema, "Angalia ulifanya nini. Wewe sio wangu tena!" Hakuna babu wa upendo ataweza fanya hivyo.

Bwana alinionyeshea kupitia uzoefu huo, "Daudi, unaruhusu upendo huu kwa mtoto huyu. Lakini wakati mwingine huruhusu mimi kukupenda kwa njia ile ile. Unajivunia saana watoto wako, lakini wakati mwingine umeshindwa kuniruhusu kujivunia ndani yako.”

Nikasikia Bwana akisema neno la huruma kwa moyo wangu. Alisema, "Mwanangu, unanibariki, unabariki moyo wangu!" Hakuna mtu aliyewahi kusema kitu bora kwangu katika maisha yangu. Tena najua neno hili ni kweli. Mungu hufurahia watoto wake (Zaburi 147:11).