Mungu Hatawahi Kamwe Kuwaacha Watu Wake

Kwa kuwa BWANA huwapenda wenye haki naye hatawaacha waaminifu wake. Watalindwa milele, lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali, (Zaburi 37: 28).

Katika kitabu cha Luka 22, Yesu atoa Onyo kali sana kwa mfuasi wake mkuu. Yesu alimwita Mtume Petero kando na kumueleza kinaga ubaga: ““Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe…” (Luka 22: 31 – 32).

Wakristo wachache watashangazwa na hilo jambo, kwamba Shetani alitaka kumtia Petero majaribuni. Tunajua, Petero alikuwa mkuu wa Mitume. Kwa wasomi wa Biblia, si ajabu Shetani kuomba ruhusa ya kuja kinyume na huyu Mtume jasiri. Biblia ina nakili wazi kuwa azma ya Shetani ni kuvunja Imani ya wale wamtumikiao Yesu. Kwa wale Mitume kumi na wawili, Petero ajitokeza wazi kama Yule angeweza kutetea Imani yake ndani ya Kristo.

Walakini, kuna jambo kwa hili nano linalotatanisha wakristo. Ni hili: Mungu alimruhusu Shetani kumjaribu Petero! Ndio, Mungu wetu wa Mbinguni alimkubalia Shetani kumsumbua mtumishi wake wa dhamana.

Fikiria haya: Yesu alikwisha sema, Juu ya Maneno ya Petero aliyotamka kwa Imani, atalijenga Kanisa lake. Na sasa, Kristo aliweka Neno lake taabani kwa kumuweka Petero ndani ya miale ya Shetani. Tunajua, hata ingawa Petero alikuwa jasiri, alikuwa na kasoro pia.

Je, Petero angelianguka mtihani huu? Kristo angelijenga vipi Kanisa lake juu ya Maneno ya yule atetemeshwaye na Shetani? Zaidi ya hayo, ingelikuwaje Mungu mpenzi amuelekeze mpendwa wake kwa majaribu kama haya? Wakristo watatanishwa na mambo haya.

Kwa waumini wengine, jambo hili kumhusu Mungu Baba halieleweki.

Kwa wengine Kanisani, jambo hili ni zito sana kujaribu kulinganisha na Mungu. Walakini, Biblia inatueleza kuwa yaliompata Petero yamekwisha wapata wengi wapendwa wa Mungu.

Tuchukuwe mfano wa Ayubu, tafakari yale mwenye Haki Ayubu aliyopitia: kupoteza mali yake, nyumba, na hata watoto wake wa dhamana. Ndio maana Ayubu alipopitia mambo haya, wenzake wampendao Mungu walishangaa. Hawange kubali kuwa Mungu angelimruhusu Shetani kumtia majaribuni muumini wake. Katika mawazo yao, Ayubu lazima alikuwa ametenda mambo maovu yaliyomletea mikasa.

Lakini, Hakuna lile lisilo mbali na Ukweli! Katika Mlango wa kwanza wa kitabu cha Ayubu, Shetani aliingia Mbinguni kuomba ruhusa ya kumtia Ayubu katika majaribu. Mungu alimkubalia! Alimpa Shetani ruhusa kumtia mwanadamu mwenye haki katika majaribu makali mno yaliomsukuma mpaka mipakani mwa Imani yake.

Wapendwa, katika kila jambo, Biblia inanakili waziwazi: Njia moja tu ambayo Shetani hupata kujaribu Imani ya wana wa Mungu – hata Ayubu na Petero – ni kupitia ruhusa apatayo kutoka kwa Mungu Baba. Naye Mungu hageuki, Neno lake ni lile lile jana, leo na hata milele (soma Waibrania 13:8). Kwa hivyo, tunaweza kuwa na hakika kuwa kama vile ilivyowatendekea wale wapendwa, itamtendekea yeyote Yule anayekiri kumfuata Yesu.

Lakini hebu tazameni, Ukweli huu: Shetani hawezi kutikisa Imani ya mtoto wa Mungu bila ruhusa kutoka Mungu mwenyewe. Neno hili llinatuambia nini? Kwa ufupi: Mungu ana sababu mwafaka na mpango maalum kwa majaribu yote ya Shetani maishani mwetu.

Na kweli, Yesu alipomuonya Petero, Alimtia moyo kwa maneno haya ya ajabu: “...nimekuombea… ili imani yako isishindwe” (Luka 22:32). Kwa wazi, Kristo alijua Petero atashinda majaribu haya, Imani yake ikisimama Imara. Ili laamanisha kuwa, Yesu alikuwa na mpango mwafaka na Maisha ya Petero, kupitia majaribu hayo.

Mambo haya ni kweli kwetu, Yesu ameahidi kuombea Wafuasi wake, sio Petero tu lakini wote wale wanao mfuata katika vizazi vyote. Bwana wetu yuko na mpango kwa kila jaribu tupatalo.

Tafakari maonyo ya Krisot katika maandiko.

Ufunuo unatuambia kuwa Shetani amekuja chini duniani nyakati hizi za mwisho, kwa hasira kwa kuwa siku zake ni chache. Kwa sasa yuko vitani na wateule: “Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo Shetani ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!’(Ufunuo 12:12).

Tunaambiwa kuwa adui wetu Shetani anzurura kama Simba, akitaka kumeza: “Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu Ibilisi, kama simba angurumaye huzungukazunguka akitafuta mtu ili apate kummeza” (Petero wa kwanza 5:8). Kwa ufupi, njama ya Shetani ni kula na kumeza Imani ya Wateule wa Mungu.

Pia, tunaelezewa kuwa Shetani huja kama mwizi kwa wale wanao amini: “Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. (Johana 10:10). Mwizi kama huyu haibi tu bali anavunja na kumaliza kabisa Imani ya watu.

Mwishowe, tunaelezewa kuwa Shetani huleta gharika kwa watu wa Mungu, akitamani kufagia Imani yao kupitia Uoga mkuu na vita vikali: “Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko” (Ufunuo 12:15).

Mambo haya yanashutua mno. Kwa wazi, Petero aliitaji maombi ya Yesu ili Imani yake iweze kusimama imara. Walakini, ni kana kwamba Petero alikuwapuuza haya.

Kwa Ujasiri wake, Petero aliamini kuwa Imani yake itastahimili majaribu ya Shetani.

Wakrsito wengi hukumbuka majivuno ya Petero kuhusu Imani yake: “Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani na hata kifoni.” (Luka 22:33). Yale anenayo Petero kiujasiri yanaweza kuonenakana kama Ujasiri wa Kiroho. Lakini, kwa kweli, inalinganishwa na Ujasiri wa kimwili tu, ndio maana Paulo akalionya Kanisa: “Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.” (Wakorintho wa kwanza 10:12).

Paulo asema, ni lazima tuwe wanyenyekevu katika vita vya Kiroho. Yuda anakili haya alipoandika: “Lakini hata Malaika Mkuu Mikaeli alipokuwa anashindana na ibilisi juu ya mwili wa Mose, hakuthubutu kumlaumu, bali alimwambia, “Bwana na akukemee!” (Yuda 1:9). Neno la Mungu li wazi kuhusu umuhimu wa Kunyenyekea.

Hata hivyo, wakristo wengi husahau. Nishawahi kusikia waumini wakisema, “Niko tayari kutoa maisha yangu. Haijalishi nitapitia nini. Niko tayari kufa kwa ajili ya Bwana wangu.” Petero alijivunia vivyo hivyo. Lakini saa ilipofika, hakuwa tayari. Pale Petero alipokumbwa na nafasi nzuri ya kufa kwa ajili ya Kristo, alifanya jambo ambalo hakuwahi kudhania hapo mbeleni. Alimkana Bwana Yesu.

Katikati ya vita, pale Petero angelikiri Imani yake ndani ya Krsito, alilaani. Katika giza la uoga na dhiki, Mtume huyu alinena mbele ya wote pale, “Sikuwahi kumjua Mtu huyu!” jameni ni wakati mgumu vipi ulikuwa kwa Petero? Mjasiri mkuu wa waumini alishushwa mpaka kuwa muoga, akiogopea maisha yake.

Ninahakika ya kuwa, wakristo wengi huamini kuwa hawawezi kutenda dhambi kama hii ya Petero. Wao hujiambia, wako juu ya dhambi kama hii. Wanajiona wakimfuata Yesu mpaka kufa. Nina Jambo muhimu la kuwaambia waumini hawa: hakuna mkristo yeyote anayeishi leo aliye juu ya makosa ya Ayubu au Petero. Pale majribu makali yanapotujia kutoka kwa muovu, kama vile yalivyo wakumba watu hawa, sote hukumbwa na mkasa wa kutikiswa kwa Imani.

Sitaki kumshtua yeyote Yule, kwa matamshi yangu kuwa sote tunaweza kuanguka.

Nataka tu nisisitize hili kwa kuwa ni jambo muhimu mno. Biblia iwazi, nami nawaona waumini wengi walio karibu kukata tama.

Mimi najmjua Mtumishi mmoja mpendwa ambaye Imani yake imetikiswa. Ninaongea kuhusu waume na wake wa Imani kuu. Wale wanao Ubiri na kutenda uponyaji na miujiza. Hawa ni Wateule ambao singefikiri ya kuwa wangemshuku au kukosa kumuamini Mungu. Nilikuwa na hakika, “kama kuna Yule awezaye kupitia gharika, tazama huyu ni Mtumishi wa Mungu awezaye hayo!”

Lakini, waumini wengine sasa wanashuku hata kama Mungu kweli hujibu Maombi. Wakati mmoja Imani yao ilikuwa kuu iliimarisha Imani ya wengine. Lakini sasa, kama Ayubu na Petero, majaribu makali yamewakumba, wamejikuta katika vita wasivyoweza kustahimili, na wameanza kulegea.

Pale Petero alipokuwa katikati ya vita hivi, Yesu alikuwa akimuombea. Jameni, kwangu mimi, hili ndilo Neno la kutia moyo sana ndani ya Biblia yote: “Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe,” (Luka 22:32). Tafakari yale Yesu alikuwa anamueleza Petero. Alimhakikishia kuwa, lolote atakalo pitia, - haijalishi ni jambo gani hilo, hata kama ni kumkana Krsito – Imani yake Haitazimia.

Kwa kweli, Petero hakuwa ameachwa na Mungu – ata kwa dakika moja. Hakuachwa ata alipo mkana Kristo na kutoroka. Yule aliyekuwa Jasiri, sasa alivunjika kwa makosa yake, hakuwahi kuwa pekee hata kidogo. Wapendwa nasi pia ni vivyo hivyo.

Haijalishi majaribu yanayokukumba – iwe ni uchungu gani unayopitia, jaribu unalopitia, makosa gani unayowaza.

Wakati huu – katikati ya gharika, uchungu na majonzi – Yesu anakuombea. Anakupigania. Na hajawahi kukuacha peke yako.

Tafakari neno la kutia moyo; Yesu alimueleza Petero, pamoja na Onyo. “nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.” (Luka 22:32). Neno hili laja pale tu Yesu alipomueleza Petero kuwa atapepetwa, kwa kweli, maneno haya yote yako katika mstari mmoja!

Wapendwa, hili ndilo himizo la kutia moyo kwetu sote. Mungu muumba ametushikilia mikononi mwake. Anatueleza, kama vile Petero, “Amka, nenda sasa. Usibaki kwa makosa yako. Bali, enenda ukawalishe kondoo wangu. Nenda ukawaonya wapendwa wangu kuhusu mbinu za muovu dhidi yao. Waeleze nimewashikilia kwa mikono yangu, katika majaribu yote.”

Kwa ufupi, Petero alikuwa na kazi muhimu ya kufanya. Na alikuwa na ujuzi mkuu kuhusu Neno alilopaswa kuhubiri. Jua kwamba, Yesu aliambia Kanisa kuwa hatuweza kutojua au kupuuza mbinu za Shetani. Petero angeliweza basi kuwaeleza waumini, sio tu majaribu watakayopitia, lakini pia vile Mungu muaminifu atawaokoa kutoka hata kwa majaribu makuu.

Lazima tujuwe kwa hakika mbinu na mipango ya adui. Na silaha kuu zaidi anatumia Shetani ni Uongo – Uongo mkali kinyume nasi, kutoka kwa mdomo wa baba wa Uongo! Uongo wake mkuu ni upi? Kwamba Mungu si muaminifu kwa watu wake.

Kama vile alivyo fanya tangia jadi, Shetani huomba ruhusa kutoka kwa Mungu atupepete leo. Anataka kupiga Nyumba zetu, Ndoa zetu, Watoto wetu, Afya zetu, Kazi zetu, Ujuzi wetu, na Imani yetu ndani ya Bwana. Hii ndio gharika ambayo Ufunuo unanena: Gharika ya majaribu kinyume na Imani yetu.

Unaweza labda kushangaa: “Kunaweza kuwa kubaya kiasi gani kwa Muumini? Mungu hurusu mpaka wapi anapo kubali tupepetwe? Nitawaelekeza kwa Waibrania 11, pale tunasoma majaribu yaliowakumba wajasiri wa Imani. Neno lasmea, “Hawa wote walishuhudiwa vema kwa sababu ya imani yao” (Waibrania 11:39).

Masumbuko waliopitia hawa majasiri wa Imani, ndio yale tunayopitia hata leo.

Natafakari Wakristo walio kule Iraki, wanaopitia mambo yakushtua Imani yao katikati ya vita. Wengi wao iliwabidi watoroke kuokoa maisha yao, wakiacha nyuma nyumba zao, kazi na Kanisa. Ili wanusurike, ilibidi wakimbie Asiria, Yordani na miji ya kando ambayo pia hayana urafiki na Wakristo. Hawa waumini kutoka Iraki hawana kazi wala makao, hawana pa kutorokea. Lazima waombe kila siku kupata chakula. Wengi wameuawa. Hata hivyo, wanaendelea kuubiri Injili katika nchi hizi za ukimbizi pale wametorokea kwa sababu ya vita.

Nimekwisha pata habari kutoka wa waumini hawa kutoka Iraki. Wameandika, “Ndugu David, Majaribu si eti yanakuja, kwetu sisi, majaribu makali yamekuwa nasi kwa miaka mingi sasa.” Wameona taabu tangu jadi, wameelewa kukwamilia Imani. Kama Petero, wametengwa Kuubiri na nguvu, wakilionya Kanisa la Kristo.

Mimi naamini kwa kweli, wengi wetu tuko katika majaribu makali kutoka kuzimu, tunastahimili majaribu ya kishetani. Je wewe? Kama hujapatwa na jaribu la Imani? Ninakusihi: shukuru Mungu. Lakini, nyenyekea, usiwahi kujisifu kuwa Imani yako ni ya nguvu kuliko wengine.

Shetani hungojea mpaka pale anayejaribiwa amevunjika moyo, na kuisha nguvu. Yeye hungoja mpaka pale maombi yana kaa kana kwamba hayajibiwi – pale matumaini yamekwisha kabisa, pale ambapo mbinu zetu zimekwisha. Hilo ndilo lilimtendekea Petero, alipomuona Bwana wake akiteswa mbele ya kikao cha Mafarisayo. Iilimtendekea Ayubu, aliye lazimika kuwaza alipo poteza kila kitu cha muhimu kwake.

Maswali yanapochipuka akilini mwa anaye pitia majaribu – “Mungu, ukowapi? Kwanini maombi yangu hayajibiwi?” – papo ndipo Shetani huchagua kupanda Uongo wake: “Mungu amekuacha. Amejitenga nawe. Hakusikii.”

Kumbe Mungu hajakuacha – na hatawahi kukuacha. Kwa kweli, sasa hivi anakuambia hivi: “nimekuhakikishia sitakuacha kamwe. Sasa basi, simama, enenda ukalishe kondoo wangu. Chunga mbinu za Shetani kinyume nawe, tazama, niko nawe, hata mpaka mwisho wa Dunia.” Amina!

(Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)