MUNGU ANA MPANGO KATIKA KAZI

David Wilkerson (1931-2011)

Mpendwa, ni muhimu kufahamu kama watu wengine wanaangalia maisha yako na kuathiriwa na tabia yako. Kwa hiyo, nauliza, Je!Unamwenendo gani katika tabia yako? Je! Watoto wako wamewekwa ndani Kristo kama wanavyoona mwenendo wako? Je! Wakristo wenye kiwango cha chini wanavutiwa kumjua vizuri zaidi kwa sababu ya ushuhuda wako? Je! Wenye dhambi wanavutiwa na Yesu kwa sababu ya majibu yako ya upendo? Unapokutana na changamoto katika kutembea kwako kwa kila siku, je! Una harakia kunyenyekea Roho Mtakatifu? Au je, wewe hulalamika na kumlaumu, na hatimaye kuwa kimya kwa Baba yako wa mbinguni?

Majaribio yako yote yamepangwa kukupeleka mikononi mwa Yesu, hukua ndani yako radha nzuri ya uaminifu na imani katika Bwana wako. Tuna tabia ya kusahau mambo yote mazuri ambayo Mungu ametufanyia, hivyo ni vizuri kukumbusha wenyewe ushindi wa zamani na uingiliaji wa Mungu. Au tunaweza kufikiria kwamba changamoto ya hivi karibuni ni kali sana, na tunasema, "Ee Mungu, wakati huu ni vigumu sana kwangu kuvumilia." Na Mungu anajibu, "Angalia nyuma tu na kunikumbuka." Hivi ndivyo Daudi alifanya kabla ya kwenda nje na kumshinda Mfilisti mwenye nguvu.

"Daudi akasema, 'Bwana, aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa mfilisti huyu'" (1 Samweli 17:37).

Wakati mwingine Daudi akasema, "[Bwana] akanitoa akanipeleka panapo nafasi, aliniponya kwa kuwa alipendezwa name. Bwana alinitendea sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa" (Zaburi 18:19-20).

 Ikiwa unasikia kama wewe unadhibiwa na Mungu, hakika kuwa ni kwa sababu anafurahia kwako na ana mpango katika kazi. "Nami niliaminilo ndilohili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu" (Wafilipi 1:6).