MUFANO HALISI WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Katika Agano la Kale, watu wa Mungu walimwacha mara kwa mara, lakini kila wakati aliwarejesha na kuwabariki sana. Bwana alikuwa na haki kubwa ya kuacha juu ya Israeli, lakini aliendelea kuwa mwaminifu kwao. Nehemiya anaandika ukweli huu wa ajabu juu ya asili ya Mungu:

"Lakini walipokuwa wamekwisha kustarehe, walitenda ma baya mbele zako ... hata hivyo waliporejea na kukulilia, uliwasikia toka mbinguni, ukawaokoa mara nyingi kwa reheme zako ... Ila kwa rehema zako nyingihukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu mwenye neema, mwenye rehema" (Nehemia 9:28, 31).

Mtume Isaya alijua hali hii ya asili ya Mungu. Kama Musa kabla yake, Isaya alihubiri juu ya hukumu ya Mungu dhidi ya dhambi. Alizungumzia siku za giza za kukata tamaa kuja juu ya wale wanaoishi katika uasi wa milele. Hata hivyo, katika moja ya ujumbe wake wa moja kwa moja, Isaya alisimama ili atowe kauli hiyi:

"Nitautaja wema wa Bwana na sifa za Bwana kwa yote aliyotukilimia Bwana; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake." (Isaya 63:7).

Kila mahali Isaya aligeuka aliona kurudi nyuma na uasi katika Israeli. Hata hivyo, licha ya hili, Isaya aliangalia ndani ya moyo wake na kukumbuka ufunuo wa kile ambacho kilikua mufano halisi wa Mungu. Naye akaanza kumsifu Mungu kwa uaminifu wake: "Ee Bwana, tulikuasi juu yako na tukageuka kutoka kwa Roho wako Mtakatifu, tuokoe tena kwa huruma yako kubwa. Kuhimiza huruma yako kwetu, umejaa wingi wa wema."

Baadaye nabii Yoeli alitoa maonyo mazuri, lakini hata kama alivyotabiri kuhusu tetemeko kubwa la ardhi na giza ya jua na mwezi, ghafla alianza kusema juu ya upendo wa Mungu:

"Mkamrudie Bwana, Mungu wenu, kwa maana Yeye ndie mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema" (Yoeli 2:13).

Wapendwa, kuna nyakati tunahitaji kukumbuka ufunuo huu wa huruma ya Bwana kwa sisi wenyewe.