MTAZAMO WA NJE

Gary Wilkerson

"Lakini mlifanya vema mliposhiriki nami katika dhiki yangu. Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua enyi Wafilipi mnajua hiyo . . . nilipoondoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lilioshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi pekee yenu. Kwa kua hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, mara si mara moja. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi katika hesabu yenu . . . Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina" (Wafilipi 4:14-20).

Kama Wakristo, mara nyingi tunfikili kuhusu ukarimu; tunapanga mpango kwa ukarimu na kutoa kwa ukarimu kwa familia yetu, kwa wake wetu, kwa marafiki zetu, kwa jirani zetu, na kwa kanisa letu na misaada mengine. Lakini Paulo alikuwa akisema kuhusu hili katika mazingira ya siri - siri ambayo watu wengine hawajui kuhusu nguvu za ukarimu.

Paulo alikuwa akisema, "Sijawahi kuhangazia kw ajili ya zawadi mliyonipa. Nimekuwa nikiangazia kwa jambo ambalo ninaona linafanya kazi ndani yenu wakati munanipa."

Je, unaona tofauti huko? Angeweza kusema, "$50 ambayo mumenipa zitakwenda kununua chakula cha wiki tatu. Mungu asifiwe!"

Nina hakika angeweza kushukuru kwa sababu hiyo, lakini unajua nini kilichopita kwa mawazo yake? Alidhani, "Mungu Asifiwe! Injili inafanya kazi ndani yako kwa sababu hujishughulisha kamwe. Hauishi katika wasiwasi, unashikilia mambo mwenyewe. Huna hata kuishi katika mgawanyiko na mtu mwingine. Unawapa watu! Unaishi maisha yako kwa mtazamo wa nje na kufanya mambo ambayo huwezi kufanya kama injili haijawa mizizi moyoni mwako."