MIPANGO YAKO NI BURE?

David Wilkerson (1931-2011)

"Injili hii ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kama ushuhuda kwa mataifa yote; na ndipo mwisho utakuja" (Mathayo 24:14).

Wengi kanisani leo wanajaribu kuamua ukaribu wa kurudi kwa Kristo kwa kusoma ishara za nyakati; kwa mfano, kurudi kwa Wayahudi Israeli. Yesu anasema wazi kuwa mwisho utakuja tu baada ya injili kuhubiriwa kwa mataifa yote kama ushuhuda.

"Uthibitisho wa ukweli" ni ufafanuzi wa neno la Kigiriki ambalo hutumika kwa "ushuhuda" katika msitari hapo juu. Kristo hasemi juu ya kuhubiri injili tu lakini akiwasilisha kama ushuhuda. Anasema kwamba injili tunayohubiri ni nzuri tu ikiwa imeungwa mkono na maisha ambayo yanashuhudia ukweli wake.

Mtu angefikiria kwamba Amerika, na maelfu ya makanisa ya kiinjili, ingewasilisha ushuhuda wa injili kali. Katika jiji moja kubwa kusini, kuna makanisa ya kiinjili zaidi ya 2,000. Lakini nyingi za makanisa haya yameelekeza injili ya kweli ya Kristo kwamba ufalme mdogo wa Kristo unaangaza katika maisha ya watu.

Watumish wengi mno, wadogo na wakubwa, wanaendesha kote ulimwenguni kuhudhuria semina, mikusanyiko na "kundi la kujadiliana", wakitafuta ufunguo wa kujenga huduma kubwa. Wataalamu wa huduma ya vijana wamejiandaa na chati, na kupiga kura wakati wakisikiliza mihadhara ya jinsi ya "kukuza kanisa lako." Bado wengine huhamia kwa "uamsho" wakitumaini kujifunza njia mpya za kuwezesha Roho Mtakatifu kutelemukia kwenye mkutano wao.

Kama mashirika za umisionari zinatuma wafanyikazi zaidi, wamishonari wengi sana wanakuja nyumbani ndani ya miaka michache tu, wamekatishwa tamaa na kupigwa chini kwa sababu hawakuendeleza ujuzi wenyewe wa ukuu wa Kristo au utimilifu wa Roho Mtakatifu. Kuna hitaji la watu waliohitimu zaidi kushinda mataifa kwa ajili ya Kristo lakini uwepo na upako wa Roho Mtakatifu tu ndio utaleta mafanikio ya kudumu. Injili ya Yesu Kristo itahubiriwa kama ushuhuda - na ndipo Bwana atakapokuja!

Mpendwa, mipango yako ni bure ikiwa Yesu hajawekwa kiti cha enzi katika kila eneo la maisha yako. Unapopata maarifa, na kutumia maoni na mikakati mipya, hakikisha maisha ya Kristo yanakaa ndani yako.