MIONGOZO MIWILI YA KUTEGEMEA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Hakuna mwongozo wa kuishi kabisa kwa kutegemea Bwana, lakini kuna miongozo rahisi ambayo unaweza kufikiria. Kwanza, kuwa na uhakika kwamba Bwana anahamu na nia ya kufanya mapenzi yake ajulikane kwako, hata katika maelezo mafupi ya maisha yako. Roho Mtakatifu anayeishi ndani yaku anajua mapenzi ya Mungu kwa ajili yako na atakuelekeza, atakuongoza na atazungumza na wewe.

"Lakini yeye atapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza katika ukweli wote ... Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari" (Yohana 16:13-14). Yesu anatuambia kwamba Roho Mtakatifu atatuonyesha akili na mapenzi ya Mungu. "Asikiapo [sauti yako], ndipo atakapojibu ... Masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, 'Njia ni hii, ifuateni'" (Isaya 30:19, 21).

Unaweza kuwa katikati ya taabu au mateso kama matokeo ya uamuzi wa haraka. Bwana anakuahidi, "Sikio lako la ndani litasikia Roho wangu akizungumza na wewe, 'Nendeni kwa njia hiyo. Fanya hili. Usifanye hivyo."

Pili, tunapaswa kuomba kwa imani isiyo tingizika yenye kuwa na nguvu ya kutii mwongozo wa Mungu. Andiko linasema, "Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenywe shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Kwa maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu chochote kutoka kwa Bwana" (Yakobo 1:6-7).

Wakati Mungu anatuambia tufanye kitu furani, tunahitaji nguvu ya kuikalia somo na kumtii kikamilifu. Shetani na mwili daima watazaa mashaka na maswali, na tunahitaji nguvu kutoka mbinguni sio kusema "ndiyo" kwa hali ambapo Yesu amesema "hapana."

Wakati unapokuwa hawuna uhakika wa kutambua sauti ya Mungu, umfikie kwa imani. Omba, msii, kulia haitosha ikiwa huamini kwamba Roho Mtakatifu atakuongoza. Mungu hawadanganyi watu wake na atafanya mapenzi yake awe wazi kwako wakati unapomtafuta.