MFANO MZURI WA IMANI KATIKA SHIDA

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati Paulo aliandika barua yake kwa Wafilipi, alikuwa ndani ya jela huko Roma, miguu yake ilikuwa imefungiwa kwa askari au kwa upande mwingine. Hali ilikuwa mbaya na Paulo aliteseka sana, kwa kutokuwa a wakati akiwa peke yake na kutukuwa na uhuru.

Fikiria hilo. Hapa kulikuwa na mtu ambaye alikuwa akifanya kazi sana, akipitia barabara kwa wazi, na kwenye bahari kubwa ili akutane na kufanya ushirikiano na watu wa Mungu. Paulo alifurahia sana kutembelea makanisa aliyoanzisha katika eneo hilo la ulimwengu. Lakini hapa alikuwa amefungwa minyororo, kwa kweli ilikuwa amefungiwa kwenye shida zaidi, mahari panaishi watu wabaya.

Baadhi ya Wakristo waliomjua Paulo walianza kunung'unika kwamba alikuwa akileta aibu juu ya Injili kwa sababu ya hali yake. Lakini Paulo alikuwa na lengo la kupata nia ya Mungu iliomruhusu kufikia hapa. Badala ya kuuliza, "Kwa nini hili lilitokea kwangu?" Aliamua kugundua jinsi majibu yake yanapaswa kuwa. Mtumishi huyu wa Mungu aliludia mawazo yake: "Siwezi kubadilisha pale nilipo lakini ninajua hatua zangu zinaamriwa na Bwana. Kwa hiyo, nitamtukuza Kristo na kuwa ushuhuda wakati mimi niko katika minyororo hii."

"Sasa Vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yagu, au ikwa kwa mauti yangu" (Wafilipi 1:20). Paulo hakuwa na njia yoyote ya kujiuzulu au kutofautiana na hali yake, lakini alikuwa amedhamiria kwamba Neno la Mungu litathibitishwa na musimamo wake katika shida yake. "Jua kwamba nimechaguliwa kutetea Injili ... Kristo anahubiriwa; na katika hayo ninafurahi, naam, nami nitafurahi" (1:17-18).

Mtazamo wa Paulo ni mufano muzuri wa jinsi tunapaswa kukabiliana na hali hizo. Inawezekana kupoteza maisha yetu yote kesho kwa kuwa nawasiwasi ya kusubiri kutolewa kutoka katika mateso yetu, lakini ikiwa inakuwa lengo letu, tutaweza kukosa miujiza na furaha ya kutolewa katika kesi yetu. Neno la Paulo kwa Wafilipi lilikuwa, "Furahini katika Bwana daima. Tena nasema, furahini!" (4:4). Nawaambia, "Furahini akatika Bwana daima!"