MBALI NA UPENDO WA YESU

Gary Wilkerson

Waanadini wana tabia ya kuzingatia giza badala ya nuru. Nasikia Wakristo wengi wanaachilia maneno maumivu: "Utamaduni ni wa kulaumiwa," au "Serikali ni yakutenda kosa," au "Kundi hilo lina ushawishi mbaya kwa maslahi yawo maalum," Ikiwa unatembea kama Yesu alivyofanya, hutaweza kulaani giza kwa sababu wewe unaangazia nuru yenye unaleta. Hebu aca nionyeshe.

Fikiria kukaa wakatika wahuduma ya kanisa alafu taa zikazimwa ghafla na eneo lote likajaa giza. Ikiwa mtengenezaji wa mataa atarudi nakuasha taa moja tu katika chumba hicho, mara moja kila mtu huonekana katika kongamano hilo, bila kujali mahali ambapo limewekwa. Rafiki, hiyo ni picha yako katika ulimwengu ulio na giza kabisa. Bila kujali ukubwa wa giza hilo, mwanga wako unaweza kuonekana kwa kila mtu katika majilani wako. Haliwezi kujificha, kwa hiyo basi aca liangaze! Kisha hakuna haja ya kuingizwa katika mazungumzo yaliyotisha kuhusu utamaduni wetu.

Aina hii ya kutembea sio tu inakuchochea katika njia ya dini lakini inakupeleka kwenye upendo wa Yesu. Hilo kamwe hutokea kama matokeo ya utendaji wa dini. Kama Yohana anatukumbusha, "Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza" (1 Yohana 4:19).

Ikiwa tunajaribu kukamilisha kazi ya Mungu kwa nguvu zetu wenyewe, mbali na upendo wake, hakutakuwa na nguvu yoyote nyuma yake. Paulo anasema, "Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao" (1 Wakorintho 13:1).

Kwa upande mwingine, upendo wa Kristo unatupa punda kila mahali, na nguvu ya milele ya mbinguni nyuma yake: "Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; ijapo ile iliyo kamili, [upendo], iliyo kwa sehemu itabatilika." (13:8-10).