MATUNDA YA UPENDO WA BABA

David Wilkerson (1931-2011)

Upendo wa Mungu ulitolewa kwetu kupitia Yesu Kristo. Kwa mujibu wa Yohana, upendo wote wa Mungu unakaa ndani ya Yesu: "Kwakua katika utimilifu wake sisi sote tulipokea” (Yohana 1:16). Unaweza kuuliza, "Ni jambo gani muhimu kwa kujua kwamba upendo wa Mungu ulitolewa kwetu kupitia Kristo? Hii inathirije maisha yetu ya kila siku?"

Ujuzi huu ni zaidi ya ufahamu wa kibiblia. Kujua kwamba upendo wa Mungu hutolewa kwetu kupitia Yesu, na una kila kitu cha kufanya na jinsi tunavyojiweka katika upendo wake. Unaona, haitoshi kwangu kujua kwamba Mungu atanipenda daima na hawezi kuacha kunipenda kwa kupitia majaribio yangu yote. Pia anataka upendo wake uwe na matokeo fulani juu yangu.

Hivyo, Kwa kweli, niaje upendo wa Mungu huleta matokeyo ndani ya maisha yetu? Hatuwezi kuangalia kwa mfano wa mtu. Kuna Wakristo hawana nidhamu ambao watageuza ufunuo wa upendo wa Mungu kuwa leseni ya dhambi. Wanajihakikishia wenyewe kwa kusema, "Mungu ananipenda upendo isina na masharti. Anaendelea kunipenda licha ya kunywa pombe kwangu, kuwa muzinzi na kuwa myenye kutafuta raha tu … neema yake ni kubwa kuliko dhambi zangu.” Watu kama hao wanafanya hivyo licha ya upendo wa Mungu.

Tunapaswa kumtazama Kristo kama mfano wetu. Yesu tayari ametuambia Baba anatupenda kwa njia ile ile aliyompenda Mwana. Hivyo, upendo wa Baba ulikuwa na athari gani kwa Yesu? Matunda ya upendo wa Baba alikuwa ndani ya Yesu wakati alitowa mwili wake kama dhabihu ya maisha kwa wengine.

Yohana anaandika, "Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwajili yetu" (1 Yohana 3:16). Hapa ilikuwa matunda ya upendo wa Mungu ndani ya Yesu. Alijitoa mwenyewe kama dhabihu kwa wengine. Nusu ya pili ya mstali huu inatuambia kusudi la upendo wa Mungu katika maisha yetu. Inasema, "Imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu" (3:16). Upendo wa Mungu hutuongoza pia kutoa miili yetu kama dhabihu ilio hai.