Maneno ya Kutuliza Yenye Matumaini

Yesu alikuwa akihutubia umati mkuu pale ambapo watu walianza kuwa na njaa. Alimtwaa mtume Filipo na kumuuliza swali muhimu. “Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?” Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya (Yohana 6:5–6). Yesu alikuwa akisema, “Filipo, maelfu ya watu wana njaa. Niambie, tutawalisha namna gani? tufanye nini?” Jameni ni mapenzi ya aina gani kutoka kwa Kristo. Alikuwa anajua lakufanya; biblia inatueleza hivyo. Alikuwa anamfunza Filipo jambo muhimu. Funzo hilo lina umuhimu sana kwetu haswa nyakati hizi tulizoko. Wakati huu Dunia inatikiswa kushinda nyakati zingine zote katika historia. Misukosuko hii imekuja pale Wakristo kote duniani wanapitia majaribu makuu. Maelfu wamekaa usiku mzima wakijaribu kuwaza shida zao. “Labda hili litafanya kazi – hapana, hapana. Labda hili ndilo suluhisho – hapana, hilo halitafanya kazi. Nitafanya nini?” Yesu alipomuuliza Filipo hilo Swali, Wafuasi hawakuwa tu na shida ya mkate. Walikuwa na shida ya mtambo wa kutengeneza mkate, shida ya pesa, shida ya kutawanya, shida ya usafiri na shida ya masaa. Ukiunganisha kila kitu, walikuwa katika shida ambayo wao wenyewe hawangeliweza kudhania. Walikumbwa na jambo lisilowezekana.

Wapendwa, tafakari haya: ni katikati ya janga lako kuu, Yesu akaja na kukuuliza, “tutafanya nini kuhusu jambo hili?” Anajua kamili lile atakalofanya. Yuko na mpango. Lakini angependa kujua tu vile wewe ungelifanya. Jibu sawa kutoka kwa Filipo lingekuwa, “Yesu, wewe ni Mungu. Hakuna husiloweza kufanya, kwa hivyo nimekukabidhi shida hii, sasa si shida yangu tena bali ni yako.” Kupita mambo yote, Yesu alitaka Filipo akumbuke maneno ambayo alikuwa amekwisha waeleza mbeleni kuhusu Uaminifu wa Mungu. Ninaamini Kristo angependa watu wake wote leo wawe hivyo. Ametupea maneno yenye nguvu mno, yenye kutuliza na yenye Matumaini haswa kwa nyakati kama hizi za shida. Ni sisi tijikumbushe Ukweli huu tunapopitia nyakati hizi za shida.

1. Mungu anatukumbusha, “Mimi ni Nguvu, na wa Huruma

“Kisha Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninahurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu na hawana cho chote cha chakula, nami sipendi kuwaaga wakiwa na njaa wasije wakazimia njiani.” Mathayo 15:32): Yesu anena Jambo kwa waumini katika vizazi vyote. Anatuambia, “Nitatenda kwa watu wangu mambo zaidi ya kuwaponya tu. Nitahakikisha wako na mikate ya kuwatosha. Ninahusika na mambo yote katika maisha yao. Nataka mujuwe kuwa mimi ni zaidi ya nguvu tu. Mimi pia ni Huruma. Ukiniona tu kama mponyaji au mtenda miujiza, utakuwa ukiniogopa tu. Lakini ukiniona mimi kama mwenye Huruma, anayepeana zawadi njema, utanipenda na utaliamini Neno langu.”

Ninaandika habari hii kwa kila Mkristo aliyekaribu kukata tamaa, karibu kuzimia, wewe uliyekabwa na shida wakati huu. Umekuwa mtumishi muaminifu, anayelisha wengine, anayeamini kwamba Mungu anatenda yale yasiowezekana kwa sababu ya watu wake. Lakini una Tashwishi kana kwamba Mungu hashughuliki na shida zako wakati huu. Tafakari wale walio katika mwili wa Kristo ambao umekwisha wahi kubariki na maneno ya kutuliza na ya matumaini, wale waliokosa matumaini. Umewaambia, “shikilia! Mungu ni wa miujiza, na ahadi zake ni za kweli. Usikate tamaa, yeye atakujibu.” Mimi nimekwisha peana mawaidha kama hayo mara nyingi. Walakini, hapa karibuni, Roho Mtakatifu aliniuliza, David, wewe unaamini kweli miujiza? Jibu langu lilikuwa, “Ndio, Bwana, ninaamini. Ninaamini miujiza yote niliyosoma katika maandiko. Jibu hili halikutosha. Mungu anauliza waumini swali, “Je unaamini kwamba mimi naweza kukutendea miujuza yako binafsi?” na sio tu Miujiza moja, lakini katika kila Janga na katika kila hali unayopitia.

Tunahitaji zaidi ya miujiza tuliyosoma katika Maandiko. Tunahitaji miujiza yetu ya kisasa, ya kibinafsi, katika hali ambayo hatuja wahi kukumbwa nayo hapo mbeleni. Unapokabwa na hali hii ya shida, unaamini kwamba Mungu atalisuluhisha? Unaamini kwamba atatenda miujiza kwa njia ambayo hukuwahi kukusudia? Hilo ndilo Swali Yesu alimuuliza Filipo. Ni Swali linalo hitaji Imani – Imani inayotuliza Moyo na kufanya “kukomeshwa kwa vita”. Ni Imani kama hiyo itakayoweza kutufanya tutulia ndani ya Baba, tukimuamini kwamba atatujibu kwa wakati wake.

2. “Imani Yetu wakati wa shida inatuwezesha kuwa an Ushuhuda wa “Ripoti Nzuri”

“Naam, kwa imani baba zetu wa kale walishuhudiwa. (Waibrania 11:2). Neno la kigiriki ninalomaanisha “Kushuhudiwa” linaweza kulinganishwa na “kuwa Ushuhuda”. “Baba zetu walikuwa na Imani iliyo kita Mizizi. Imani isiyotikisika iliyogeuka kuwa Ushuhuda duniani kuhusu Uaminifu wa Mungu wakati wa shida. Tafakari yale waliopitia hawa baba zetu: Gharika, Kutukanua, Pingu, Jela, Moto, Mateso, Vita na shimo la simba. Katika haya yote, Imani yao kwa Bwana haikutikiswa. Kwanini? Walikuwa na hakikisho la ndani kwamba Mungu alikuwa amefurahishwa nao. Baba zetu walijua Mungu amewafurahia, akisema, “Vyema! Mumeniamini.” “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii. (Waibrania 11:6). Tunapokwamilia Imani yetu nyakati za shida, huwa tunapokea hakikisho kutoka kwa Roho Mtakatifu: “Vyema. Wewe ni Ushuhudu wa Mungu inayopendeza”

Unapotulia ndani yake wakati wa Gharika, ukikwamilia Imani yako, unapokea “Ripoti Nzuri.” Na ndipo unakuwa ishara ya matumaini kwa wale wanaoshuhudia. Wale wanao tafakari maisha yako – nyumbani, kazini, mtaani – wanasoma kwamba Tumaini lipo hata kwao pia. Wanapokutazama vile ulivyo ndani ya shida zako, wanagundua, “pale kunasimama mtu ambaye hajapoteza Imani yake kwa Mungu. Hana uoga kamwe. Ni nini inamfanya awe wa Imani katikati ya janga? Mungu wetu amepatiana yote yanayotakikana kuimarisha Imani yetu, ata kama Janga zitaongezeka. Tumepewa Roho Mtakatifu, Anaye ishi ndani yetu na kukaa nasi, na Ufunuo wa Neno la Mungu. Yote haya yata tuimarisha, na kutuwezesha kupata Ushuhuda wa Ripoti Nzuri hata dunia inapotetemeshwa.

3. Tumepewa silaha maradufu kupinga Uoga.

Uoga unapotukumba inabidi tukumbuke Ukuu wa Mungu wetu. Inatupasa tukumbuke Ukombozi wake kwa wale wanao muamini, na kuitisha hiyo Nguvu ya Kiungu katika shida zetu. Uoga hauwezi kumkaba Muumini anaye jua Ukuu wa Mungu. Nehemia alijua haya vyema. Alitembea huku na kule pale ambapo Yerusalemu ilikuwa imezingirwa na mataifa waliokusanyika kwa vita. Waumini Mabakio walikuwa wakifanya kazi usiku na mchana kujenga ukuta wa Yerusalemu kujikinga na maadui hawa. Ililawalazimu washike nyundo kwa mkono mmoja na panga kwa mkono wa pili. Baada ya mda, Uoga uliwaingia. Walijikinga vipi na Uoga? Nehemia aliwakumbusha Ukuu wa Mungu wao: “Baada ya kuona hali ilivyo, nilisimama na kuwaambia wakuu, maafisa na wengine wote, “Msiwaogope. Mkumbukeni Bwana, ambaye ni mkuu mwenye kuogofya, piganeni kwa ajili ya ndugu zenu, wana na binti zenu, wake zenu na nyumba zenu.’’(Nehemia 4:14).

Hivi ndivyo Musa alikabidhi Uoga ndani ya waisraeli: “Mnaweza kujiuliza wenyewe “Mataifa haya ni yenye nguvu kuliko sisi. Tutawezaje kuwafukuza?’’ 18Lakini msiwaogope.Kumbukeni vema jinsi BWANA Mungu wenu alivyofanya kwa Farao na kwa wote huko Misri. …Msiingiwe na hofu kwa sababu yao, kwa kuwa BWANA Mungu wenu, ambaye yupo miongoni mwenu ni mkuu naye ni Mungu wa kutisha. (Kumbukumbu la torati 7:17–18, 21). Musa alikuwa anasema, “mutakutana na maadui wengi walio na nguvu kuwaliko. Mutatafakari vile ushindi utapatikana katika hali hii. Lakini, kumbukeni Ukuu wa Mungu. Jikumbusheni vile alivyowaokoa nyakati zilizopita na uaminifu wake katika ukombozi. “Yeye ni sifa yako, yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe” (Kumbukumbu la torati 10:21). Kama Imani yako imetikiswa, jikumbushe Ukuu wa Mungu. Kumbuka Ukombozi wake katika Maisha yako. Utaona Uoga wote ukivunjwa na ufunuo wa Ukuu wa Mungu.

4. Tuko na silaha ya kupinga sauti za kukata tamaa.

Katika shida zetu Leo, wengi wamepoteza Imani. Imani kuu zimegeuka na kuwa kukata tamaa. Wengi wanashangaa katika shida zao, “kwanini Mungu hajibu maombi yangu? Je, nimefanya kosa? Sielewi ni kwanini shida yangu inaendelea bila kukoma, je, Mungu amenikasirikia? Kuna wale ambao wame wasiliana nasi wakisema, “sina wakuongea naye, sina yule wakulia naye, nahitaji mtu ambaye nitaweza kumueleza moyo wangu.” Kawaida sisi tungependa to binadamu mwengine mwenye sura, macho na masikio kutusikiza na kutupea mawaidha.

Ayubu alipo lemewa na mikasa, alilia kwa uchungu, ‘‘Laiti kama angekuwapo mtu wa kunisikia!” (Ayubu 31:35). Alisema haya pale alipokuwa amezungukwa na wale waitwao marafiki, wale waliohuzunika kwa mateso yake. Kwa kweli, watu hawa walikuwa wapasha habari za kukata tamaa. Kwa hivyo Ayubu alimgeukia Bwana Mungu: “Hata sasa shahidi yangu yuko mbinguni, wakili wangu yuko juu. …. macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu (Ayubu 16: 19-20). Mfalme Daudi alikuwa amezungukwa na watu kila mara, alikuwa na familia kubwa na wafuasi wengi, lakini tunamsikia akilia kama Ayubu: “Nitaenda kwa nani?” Daudi awasihi watu wa Mungu kufanya vile Ayubu alifanya “Enyi watu, mtumainini Yeye, wakati wote, mmiminieni Yeye mioyo yenu, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu (Zaburi 62:8).

Wapendwa, mifano hii ni Mwito kutoka kwa Bwana. Anakusihi kutafuta mahala kimya pale unaweza kumlilia kutoka kwa nafsi yako. Ayubu na Daudi “walimwaga shida zao” walipokuwa taabani, nawe pia unaweza. Unaweza kuongea na Yesu kuhusu shida zako sasa hivi, mwambie vile imechoshwa na kufa moyo. Tangu enzi za jadi, Mungu amewajibu wote walio amini ahadi zake. Atasikia kilio chako pia, kwa Upendo na Huruma. Hata wahi kudharau kilio chako. Yeye atakupa nguvu mpya kwa kila tabu.

5. Tujipeana kamili kwa Bwana katika kila jambo

Yesu alitabiri kuja kwa shida duniani: “Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa …Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za vitu vya angani zitatikisika (Luka 21:25-26). Kristo alikuwa akieleza kwamba, “bila Matumaini ndani yangu, wengi watakufa kwa Uoga.” Bali kwa wale wanaomuamini, ameahidi kuwachunga, kuna Uhuru unaoshinda Uoga. Kwanini? Uhuru wa Ukweli huja pale tunapo jipeana kabisa mikononi mwa Bwana. Kujipeana kabisa ni tendo la Imani. Inamaanisha kujiweka chini ya nguvu zake, Hekima na Msamaha wake. Ina maanisha kuongozwa katika matakwa yake.Tukifanya hivi, Mungu ameahidi kuwa Mchungaji wetu – kutulisha, kutuvalisha na kutupea makao, na pia kuchunga Mioyo yetu kutokana na maovu.

Yesu ni mfano maalum wa kujipeana alipoenda msalabani. Kabla tu akate Roho, alilia, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho Yangu.” (Luka 23:46). Kristo aliweka maisha yake yote katika mkono wa Baba. Kupitia kitendo hicho, aliweka nafsi zote za wafuasi wake, kondoo wake wote katika mikono ya Baba. Tunapoambiwa tuweke maisha yetu katika mikono ya mtu mwengine, ni lazima tuhakikishe kuwa ana nguvu za kutuchunga kutoka kwa maadui, janga na vita. Paulo alitoa ushuhuda, “ninamjua Yeye niliyemwamini na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana Kwake hadi siku ile. (Timotheo wa pili 1:12).

6. Tuishi kila siku katika kumuhofu na kumuheshimu Bwana.

Nabii wanaonya kwamba Mungu hutikisa mataifa, lazima tutavutwa kumuhofu.

  • Ezekieli aliuliza, “Je, ujasiri wako utadumu au mikono yako itakuwa na nguvu siku hiyo nitakapokushughulikia? (Ezekieli 22:14).
  • Mungu alipo muonya Noah kujenga Safina kwa sababu ya hukumu “Noah alimcha Mungu” (Waibrania 11:7).
  • Ata Daudu jasiri alikubali, “Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe (Zaburi 119:120).
  • Habakuki alipo ona utabiri ya hukumu ya siku zijazo, alilia, “Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu, midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti, uchakavu ukanyemelea mifupa yangu, na miguu yangu ikatetemeka. Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa” (Habakkuki 3:16).

Elewa kwamba, Uoga uliokuwa na hawa watu wa Mungu sio Uoga wa kimwili, lakini ule Uoga wa Kumcha Mungu. Waumini hawakuogopa maadui wa Nafsi zao, waliogopa hukumu ya haki kutoka kwa Mungu. Walielewa vyaema Nguvu zilizo nyuma ya yale mateso yanayokuja. Hawakuogopa matokeo ya gharika, walihofu tu Utukufu wa Mungu. Kila mmoja wetu atapata Uoga siku zijazo. Lakini Uoga wetu uwe ule wa Kumcha Bwana, sio wa kimwili kuhusu kushuku ahadi za Bwana. Dunia nzima watu wamejaa Uoga wa kimwili, wanapo ona Uchumi ukidhoofika. Wanahofu kwamba gharika la uchumi litafagia yote yale wamekusanya. Hiyo ndio kilio ya wasio amini. Sisi tuko na Matumaini, kilio kama hicho hakifai kuwa na waumini.

Kama wewe ni mwana wa Mungu, Baba yako aliye Mbinguni hata stahimili shaka kama hiyo. Isaya anaonya: “Mimi, naam Mimi, ndimi niwafarijie ninyi. Ninyi ni nani hata kuwaogopa wanadamu wanaokufa, wana wa wanadamu ambao ni majani tu, kwamba mnamsahau BWANA Muumba wenu, aliyezitanda mbingu na kuiweka misingi ya dunia, kwamba mnaishi katika hofu siku zote kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu, ambaye nia yake ni kuangamiza? Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu? (Isaya 51:12–13). “BWANA Mwenye Nguvu ndiye peke yake ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu, ndiye peke yake utakayemwogopa, ndiye peke yake utakayemhofu (8:13). Tunapasa Kumhofu na Kumcha Mungu pekee.

7. Tuwe na Furaha ndani ya Bwana.

Amani tuliyo nayo inategemea kujipeana kwetu katika mikono ya Bwana, haijalishi shida tulizonazo. Zaburi inasema, “Jifurahishe katika BWANA naye atakupa haja za moyo wako. (Zaburi 37:4). Kama umejipeana Kamili kwa Bwana, atakutweka nguvu kuvuka shida zote. Lengo lake ni wewe uweze kufanya mambo yako ya kila siku bila Uoga au hofu, ukiamini tu Uchungaji wake. Kujipeana kwako kutakuwa na matokeo maalum katika maisha yako. Unapojipeana katika Uchungaji wa Mungu utaweza zaidi kuepuke misukosuko inayokuzunguka. Ukijipeana kwake, huta ogopeshwa na habari za kutisha. Hutakuwa ukijaribu kila wakati kutafakari njia ya kukwepa. Ni kwa sababu maisha yako, ya familia yako na maisha ya mbeleni yako mikononi mwa Bwana. Mchungaji wetu mkuu anajua kamili jinsi ya kuweka na kuhifadhi kondoo wake, kwa sababu anatuongoza kwa Upendo.

Nikimalizia, narudi kwa lile Swali la Yesu kwa Filipo: “Unafikiri tufanye nini?” Jameni jibu letu liwe hili: “Bwana, wewe ndiwe mtenda miujiza. Napeana shaka zangu zote na uoga wangu wote kwako. Ninapeana mikasa na maisha yangu katika uchungaji wako. Najua huta niacha nizimie. Kwa kweli, ninajua lile utakalo tenda kuhusu shida zangu. Ninaamini nguvu zako.” Amina!

---
Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)