MAHALI PA KUPUMZIKIA

David Wilkerson (1931-2011)

"Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuhiriki wa mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Kristo Yesu, ambaye alikuwa mwaminifu kwa yule aliyemteua, kama vile Musa naye alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu" (Waebrania 3:1-2).

Kitabu cha Waebrania kinatoa neno lenye nguvu, muhimu kwa wote ambao ni "washiriki wa wito wa mbinguni." Hii inamaanisha kwamba unasikia mbingu zikikuita. Hata sasa mbingu zinataka watu ambao wako huru kutoka kwa uchoyo wa mali na upumbavu wa ulimwengu huu - Wakristo ambao huamka kila asubuhi na kumsikia Yesu akiwaita. Wanaangalia yote ambayo yanawazunguka na kulia ndani, "Yesu, moyo wangu hauko hapa, hatima yangu sio hapa. Hakuna chochote katika ulimwengu huu kinachoniridhisha. Bali wewe pekee, Yesu, uko maisha yangu."

"[Yesu] alikuwa mwaminifu kwa yeye aliyemteua" (Waebrania 3:2). Uaminifu unamaanisha kuamini tu kwamba Mungu atalitunza Neno lake. Kwa maana hii, tunapaswa “kushikamana na mwanzo wa ujasiri wetu hadi mwisho” (Waebrania 3:14).

Kila wakati, majaribu yako yanapoongezeka na vita vinakua zaidi, unaweza kuwa umechoka. Kila siku, una adui ambaye yuko karibu kukuangamiza; ni mwongo na mwasi. Yesu alisema, "Ibilisi ... hakusimami katika ukweli, kwa sababu hakuna ukweli ndani yake ... ni mwongo na baba wa huo" (Yohana 8:44).

Shetani hapoteze wakati wake kwa kudanganya watenda dhambi; tayari wameshikwa gerezani na udanganyifu wake. Hapana, anawadanganya wale waumini ambao mioyo yao imewekwa juu ya Bwana. Kwa kweli, Shetani hutumia uwongo ulio wazi kabisa, wenye kushawishi dhidi ya wale ambao wamedhamiria kuingia kupumzika.

"Basi, imesalia raha ya  sabato ya watu wa Mungu ... Basi, kwa hiyo tufanye bidi kwa kuingia katika mapumziko hayo" (Waebrania 4:9, 11). "Kupumzikia katika Mungu" inamaanisha kuingia mahali pa uaminifu kabisa katika Neno lake. Ni mahali pa imani, ujasiri unaoendelea kuwa Mungu yuko pamoja nasi, kwamba Hawezi kushindwa, na kwamba atatuona hadi mwisho.

Tumia wakati na Baba yako leo na umruhusu Roho Mtakatifu atumikie mioyo yako na akuimarishe. Pata upumziko kwa nafsi yako amabayo imechoka, na kujitolea kabisa kwa Mungu.