KWISHA KUJUA

Gary Wilkerson

"Kwa maana nimwekwisha kujua hakika ya kwamba, wala yaliyo chini, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo - hata nguvu za Jahannamu hazitaweza kututenganisha na upendo wa Mungu" (Waroma 8:38).

Paulo anatupa neno lenye kusaidia kwa kushikamana hapa: Kwisha kujua. Ni ufunguo wa kuwa huru kutoka kila shaka juu ya neema ya Mungu kwetu.

Hata wakati tunapokuwa na wasiwasi mwingi, neema ya Mungu inapita kwa uhuru kutuponya. Iliyotokea kwa mwanafunzi Tomasi, ambaye aliwahimiza marafiki zake wakati wakisema Yesu alikuwa hai. Thomas anawakilisha Wakristo wengi leo. Mbele waliamini katika Kristo na walifurahi kama walimuona Mungu akibadili maisha. Lakini kisha pakaja jaribio la muda mrefu ambalo liliwaingiza kwa miaka.

Wakristo hawa bado wanaenda kanisani na kusikia mahubiri kuhusu wema wa Mungu. Lakini kitu ndani yao kimekufa na hawawezi kukifufua. Kubakia muda mlefu wa kukata tamaa kwa muda mrefu, pingamizi zisizofaa zimewapiga saana kwaundani na kwaumbali.

Je! Huyu ndio wewe? Yesu anataka kuja kwenu kama vile alivyomtendea Tomasi. Anataka kukuonyesha makovu yake kutokana na majaribio mabaya zaidi. Anataka nguvu ya ufufuo wake ili kukufufua uzima kwa namna ambayo huwezi kufanya mwenyewe. Anakuja kukushawishi kwa Neno lake la milele - kuonyesha kwa njia ya ufufuo wake kwamba hakuna chochote kitakachokuchochea kutoka kwa ufalme wake kusudi: "Wala yaliyo juu, wala waliyo chini, wala kiumbe kinginecho chochote hakitaweza kukutenga wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu" (8:39).

Kwa sababu ya neema ya upendo wa Yesu, Thomas aliamini tena na akawa mmoja wa wanafunzi wote waliofaa sana. Yesu hakuzuia kitu chochote kutoka kwa Tomasi wakati rafiki yake alihitaji kuamini tena. Yesu pia anakuita rafiki yake, na hazuii kitu chochote kukuweka katika upendo wake. Anakuletea ufufuo wako katikati ya jaribio lako, na kama vile Thomas, utaona utukufu wake tena na kushangaa.