KWA KWELI ACHA YESU AWE BWANA

Gary Wilkerson

Mungu anataka wewe kukua katika imani yako na kuja katika nafasi ya nguvu, shauku, ukomavu wa kiroho. Hata hivyo, anajua kwamba ukomavu hauji kwa juhudi zako mwenyewe; Mungu pekee anaweza kubadilisha moyo wako katika kila eneo na kukupa kukua unawohitaji.

"Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wenye tabia ya rohoni, bali kama watu wenye tabia ya mwilini, kama watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula kigumu; kwa kuwa mulikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, mimi ni wa Paulo; na mwingine, mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani?  Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; Bali mwenye kukuza ni Mungu" (1 Wakorintho 3:1-6).

Paulo anasema kweli wakati anasema kwamba Mungu hutoa ukuaji - lakini ikiwa hukua katika eneo fulani, je, ni kosa la Mungu? Hapana, Mungu sio Wakulaumiwa! Labda unapinga kazi ambayo Mungu anafanya katika maisha yako. Katika barua hii kwa kanisa la Wakorintho, Paulo anasema kwamba wivu na ugomvi ndio anasababisha kanisa kubaki kuwa mtoto badala ya kukomaa. Kwa maneno mengine, anazungumza na Wakristo wa kimwili. Wamemkaribisha Yesu kuja katika maisha yao lakini hawakuruhusu awe Bwana wa maisha yao.

Unapopokea Yesu kama Mwokozi wako na Bwana, maisha yako atabadirika - utakuwa aina tofauti ya mtu. "Kwa hiyo, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; Mambo ya kale yamepita; tazama, mambo yote yamekuwa mapya" (2 Wakorintho 5:17). Hata kile ambacho hakionekani kipya kimekuwa kipya kwa sababu yuko katika mchakato wa kutakaswa, kukugeuza na kukubadilisha!