KUWA TAYARI KUSAMEHE

David Wilkerson (1931-2011)

Inajulikana vizuri kwamba Mfalme Daudi alianguka katika dhambi mbaya, akafanya uzinzi na kuifunika kwa mauaji. Zaidi ya hayo, tunajua Daudi alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, kwa hiyo lazima alikuwa mwenye huzuni nyingi.

Nabii Nathani akamwambia, “Umeletea jina la Mungu aibu" Daudi angeweza kwenda kwa muda mrefu sana kubeba uzito wa matendo mabaya aliyoifanya na mara moja alikiri na kutubu. Hata kama alipokuwa akilia, Nathani alimhakikishia, "Bwana naye ameiondowa dhambi yako, hutakufa" (2 Samweli 12:13).

Hata hivyo, kusikia kwamba uhakika huo haukutosha Daudi. Unaona, ni kitu kimoja kusamehewa na kuwa kimya kwaupande mwingine kuwa huru na wazi na Bwana. Daudi alijua kwamba msamaha ulikuwa sehemu rahisi. Sasa alitaka kupata haki ya vitu pamoja na Mungu, ili apate kupata furaha yake tena. Kwa hiyo akasema, "Usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee" (Zaburi 51:11).

Zaburi 51 imeandikwa wakati Daudi alikumbuka hali ya huruma na uvumilivu wa Bwana. Katika mstari wa ufunguzi anaomba msamaha wa huruma wa Mungu: "Ee Mungu, unirehemu, sawasawa na fadhili zako, uyafyte makossa yangu."

Daudi alijua tu cha kufanya. Alilalamika! "Masikini huu aliita, Bwana akasikia, Akamwokoa natabu zake zote" (34:6).

"Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao ... walilia, naye Bwana akasikia, akawaponya na taabu zao zote" (Zaburi 34:15 na 17).

Ndugu mtakatifu, ushindi wako juu ya vita vyote ni kujifunza kuwa na imani hii: Bila kujali jinsi ulivyoanguka sana, unamtumikia Bwana aliye tayari kusamehe. Hakika, ana hamu ya kukuponya. Yeye ana upendo zaidi kwako kuliko vile unavyohitaji.