KUTOLAUMIWA NA YESU

David Wilkerson (1931-2011)

Kujaribia Bwana, huanza wakati Mungu anaruhusu mgogoro katika maisha yetu unaongezeka. Kwa nini anafanya haya? Yeye ni nini baada ya hayo? Bwana wetu anaruhusu hili kutokea ili aweze kupata mizizi ya mwisho ya kutoamini! Roho yake huenda katika chumba chochote cha mioyo yetu, kutafuta vitu vilivyoharibika - kiburi, kujipemda na vitu vingine vinavyozuia utimilifu wake ndani yetu.

Kwa kifupi, hii ndiyo maana ya kujaribu Mungu. Inatokea wakati waliochaguliwa, waliobarikiwa wamewekwa kwenye moto wa kupimwa, na mgogoro wao unaendelea kuongezeka kwa nguvu hadi hofu itakapowapeleka mioyo yao na wakalia, "Bwana, uko wapi? Uokoaji wangu utatoka wapi? Je, uko pamoja nami au la?

Yohana Mbatizaji alikabiliwa na aina ya jaribu ambayo inaweza kusababisha kumjaribu Mungu. Alipokuwa gerezani, lazima awe amejiuliza mahali ambapo Mungu alikuwa katika hali yake. Neno lilikuwa limemfikia juu ya mambo yote mazuri ambayo Yesu alikuwa akifanya - kuwaponya watu, kufanya miujiza, kuchukuwa umati wa watu ambao wakati moja walikua wanamfuata Yohana. Na sasa, hapa ameketi peke yake, akisubiri kunyongwa.

Yohana alikuwa amejua kwamba angepasha kushushwa chini ili Kristo apate kuinuliwa, lakini sasa mawazo yalipita kipimo kwa kufikiri kwake, "Kushushwa, ndiyo. Lakini kifo? Kwa nini ni lazima nife kama Yesu ni Mungu wa kweli? Bwana, haya ni mengi sana kuyavumilia."

Maneno ya mwisho ambayo Yesu alituma kwa Yohana yalikuwa muhimu sana: "Naye heri aweye yote asiyechukizwa nami" (Mathayo 11:6). Kristo alikuwa akimwambia mtumishi huyu wa Mungu, "Usinilaumu mimi, Yohana. Mungu ana mpango katika yote haya na anastahili kuaminiwa. Ikiwa angetaka nije na kukufunguwa, unajua kwamba ningekufikia muda kidogo tu. Kuwa na uhakika kwamba chochote kinachokuja kama hili, kitakuwa ni chakutoa utukufu wake na itakuwa ni utukufu wa milele kwako!"

Yohana alivumilia. Na hatimaye alikatwa kichwa na Herode, alikwenda nyumbani kwa utukufu uliojaa imani na heshima.