KUTENDA KATIKA HOFU

David Wilkerson (1931-2011)

"[Yesu] hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutoamini" (Mathayo 13:58). Kutoamini kila wakati kuzuia utimilifu wa ufunuo wa Mungu na baraka, na Maandiko huonyesha wazi hilo kwamba Mungu hapende hilo hata kidogo. Anatupatia mfano wa jambo hili katika hadithi ya Mfalme Asa, mfalme mwenye haki na kizazi cha Daudi ambaye alitawala juu ya Yuda (soma akaunti katika 2 Mambo ya Nyakati 14 hadi 16).

Wakati wa utawala wa Mfalme Asa, aliifuta ibada ya sanamu na akaleta uamsho kwa nchi hiyo. Kisha, watu walipokuwa wanafurahia baraka za Mungu, jeshi kubwa kutoka Ethiopia lilipinga Yuda, na kusababisha Asa kurejea kwa Bwana kwa sala, akitafuta msaada. Yuda alishinda ushindi mkubwa katika moja ya miujiza kubwa ya imani katika historia ya watu wa Mungu. Baada ya vita, nabii alikuja kwa Asa na, badala ya kumtukuza juu ya ushindi mkubwa, alitoa onyo: "Mfalme Asa, kwa kadri unategemea Bwana na kumtegemea kikamilifu, utabarikiwa. Utashinda ushindi baada ya ushindi na Bwana atakwenda pamoja nawe. Lakini ukimgeuka na kutegemea mwili wako, machafuko na shida zitakufuata."

Mfalme Asa alienda kwa uaminifu pamoja na Bwana, na Yuda alibarikiwa sana na Mungu, kama nabii alivyosema. Lakini basi mgogoro mwingine ulikuja na Yuda alishambuliwa tena. Adui huyo aliteka mji wenye kuwa kilomita tano tu kutoka Yerusalemu, mji mkuu wa Yuda, na kukata njia muhimu ya biashara ndani ya mji, ambayo ingeweza kusababisha uchumi wa Yuda wote kuanguka.

Wakati huu, Mfalme Asa alitetemeka, na badala ya kumtegemea Bwana, aligeuka adui, mfalme wa Siria, kwa kuomba msaada. Kwa kushangaza, Asa aliivua hazina ya Yuda mali yake yote na kuipeleka kwa Washami ili wa okowe Yuda - kitendo cha kutoamini kabisa. Mungu alikuwa anamawazo ya mpango wake wa kumukoa Yuda, lakini Asa akatosha mpango huo kwa kutenda katika hofu. Kwa sababu Asa hakumtegemea Bwana, tangu hapo Yuda alikuwa na vita.

Kufanya kutokuamini kila wakati kunaleta hofu na kuchanganyikiwa - hakuna tofauti. Lakini kuamini Neno la Mungu litawawezesha kusimama imara katika kukabiliana na shida zozote na kumruhusu Mungu kuleta ushindi.