KUSUBIRI MWELEKEO

David Wilkerson (1931-2011)

Sauli alimpa Mungu muda wa mwisho! Yeye hakuitangaza, lakini moyoni mwake Sauli aliamua kwamba ikiwa neno kutoka juu halikuja kwa wakati fulani, angefanya chochote kilichohitajika ili kuokoa hali hiyo.

Naye [Sauli] akangoja siku saba, kwa kadili ya muhula uliowekwa na Samueli lakini Samweli hakuja Gilgali; na hao watu wakatawanyika mbali naye. Sauli akasema, Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani. Akaitoa sadaka ya kuteketezwa” (1 Samweli 13:8-9).

Kwa kukosa subira, Sauli aliendelea mbele, akifanya dhambi akiwa kama kuhani ili atoe dhabihu. Alijua kidogo kwamba Samweli alikuwa amekalibia kushuka. Wakati nabii alipofika, alisikia alufu ya dhabihu Sauli aliyetolea na akakasirika na maovu ya kutokuwa na subira kwa mfalme kukamuletea dhambi.

Ninaamini Samweli alichelewa kwa sababu Mungu alimwambia wazi wakati wa kufika. Unaona, hii ilikuwa mtihani wa kuona kama Sauli angeamini kwamba Mungu anaweza kuaminiwa.

Mungu alifanya yote kwa sababu alitaka kumpa Sauli ushuhuda wa kujitegemea kwa unyenyekevu juu yake katika mambo yote, hasa katika mgogoro wa giza. Lakini Sauli alishindwa mtihani. Aliangalia hali mbaya na akaamua kuwa kitu hico lazima kifanyike.

Je, unaweza kujiona mwenyewe katika hali ya Sauli? Ninasikia akijiuliza kwa nafsi yake, "Siwezi kuchukua uchungu huu tena. Mungu alinipeleka kufanya kazi yake na napendelea kufa kwa ajili yake. Lakini kwa kweli ni lazima niketi hapa kufanya kitu? Ikiwa sikifanye, kila kitu kitaondoka kwa udhibiti.” Sauli alihisi haja ya kukuza kutenda mara moja katika hali hiyo. Na hatimaye uvumilivu wake ulizidiwa.

Hii ndio ambapo tunashindwa wakati fulani katika kutembea kwetu na Bwana. Kwa nyakati fulani, hatukungoja mwelekeo na tumefanya mambo kwa mikono yetu wenyewe kwa sababu hatupendi hisia zisizo na uhakika na wasiwasi. Lakini Bwana anatafuta utegemezi wa jumla. Hiyo ina maana kumwamini kikamilifu kufanya jambo sahihi kwa njia sahihi kwa niaba yetu. Na inamaanisha kumusubiri kwa subira sio kwa wasiwasi lakini kwa roho ya kutuliya.