KUSIKILIZA SAUTI YA BABA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu aliishi maisha yake hapa duniani kwa kutegemea kabisa Baba wa mbinguni. Mwokozi wetu hakufanya chochote na hakusema chochote mpaka aliposhauliyana kwanza na Baba yake katika utukufu. Na hakufanya miujiza isipokuwa yale Baba aliyoamuru. Alisema, "Kama vile Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo ninenavyo. Na ... Hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya siku zote yale yampendezayo" (Yohana 8:28-29).

Kristo alifanya hilo kuwa wazi kabisa kwamba mazoea ya utegemezi wa jumla, daima kusikiliza sauti ya Baba yake, ilikuwa sehemu ya kutembea kwake kila siku. Tunaona hili katika eneo la Injili ya Yohana ambako Yesu alimwona mtu mwenye ulemavu amelala karibu na bwawa la Bethesda. Yesu akamgeukia mtu huyo na kumuamuru achukue kitanda chake na kutembea - na mara moja mtu huyo akafanywa mzima na akaenda akiwa muzima.

Viongozi wa Kiyahudi walikasirika kwa sababu katika mawazo yao, Yesu alikuwa amevunja Sabato kwa kumponya mtu. Lakini Yesu akajibu, "Nilifanya tu yale Baba yangu aliyeniambia kufanya." Alieleza, "Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo Mwana vile vile. Kwa kuwa Baba ampendaaye Mwana, naye humwonesha yote ayatendayo mwenyewe" (Yohana 5:19-20).

Yesu alisisitiza kwa waziwazi, "Baba yangu alinifundisha kila kitu ambacho nilipaswa kufanya." Yesu katika mwili wake, alikuwa anategemea kazi ya ndani ya kila siku kutoka kwa sauti ya Baba ili imwongoze. Alipaswa kusikia sauti ya Baba yake saa kwa saa, muujiza kwa muujiza, siku moja kwa wakati.

Yesu aliwezaje kusikia sauti, sauti ndogo ya Baba yake? Biblia inatuonyesha kwamba hilo lilitokea kupitia sala. Kwa mara kwa mara, Yesu alikwenda mahali pa faragha kuomba. Alijifunza kusikia sauti ya Baba wakati akipiga magoti.

Ninakuhimiza kutumia muda na Yesu mahali pa siri ya sala. Kisha ukae kimya mbele yake na utapata ukweli kwamba Kristo peke yake anaweza kutoa kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyebarikiwa.