KUSIKILIZA MUONGOZO WA MUNGU

Jim Cymbala

Wakati tunapokuwa na Mungu, tunapaswa kutaka kufanya zaidi ya kuwasilisha orodha ya maombi - tunahitaji kusikiliza sauti yake! Mtu mmoja alisema wakati moja, "Je! Cha muhimu zaidi, tunapomwambia Mungu mahitaji yetu, ambayo tayari anajua kabla ya kumwambia, au sisi kusikiliza kwa sauti yake, kusikia yaliyo moyoni mwake?"

Najua watu wengine hawaamini kama tunaweza kuendelea kusikia sauti ya Mungu. "Tayari ilishasema chenye anachotaka kusema katika Biblia. "Wanaweza kusema kuwa kusikia kutoka kwa Mungu ni ukeleketwa wa kidini au aina ya hisia za kutisha. Lakini historia ya kanisa la Kikristo kabisa inakataa imani hiyo. Je! Watu wengine wangependa kuwa kama misionari  Muingereza Hudson Taylor - ambaye, wakati alishika muda wa kuwa na Bwana, alihisi Mungu akiita moyo wake kwenda China – Je! Amepeleka injili kwa watu hawajafikiwa na njili huko Asia? Kwa kweli, ni aje mu misionari yeyote ambaye amewahi kufanya jambo kubwa kwa Mungu amejua kufanya hivyo isipokuwa Mungu aliwaambia kwanza? Hakuna aya katika Biblia ambayo inasema, "Nenda Bangladesh!"

Ingawa sisi wote tunajua kwamba Biblia imekamilika na Mungu hazungumzii kuchukua nafasi ya mafundisho au kuzungumza juu ya kiwango hicho cha Maandiko, haendelee kuzungumza. Anaweza kutoa maneno muhimu ya onyo au kutuma ujumbe ambao una matumizi binafsi. Wakati mwingine ni neno la uongozi - mwelekeo tunapaswa kuingia. Mwelekeo wa aina hiyo husikilizwa tu kwa kusikia au moyo wa kusikia.

Mojawapo ya vifungu ni napendelea sana hupatikana katika Isaya. "Bwana Mwenye Enzi Kuu amenipa lugha iliyofundishwa vizuri, kujua neno ambalo huwasaidia wenye uchovu. Ananiamsha asubuhi baada ya asubuhi,  anaamusha sikio langu lipate kusikia kama mtu anayefundishwa" (Isaya 50:4, msisitizo aliongeza).

Jim Cymbala alianza na Brooklyn Tabernacle akiwa na wanachama wasio zidi ishirini katika jengo la chini katika sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.