KUSHIRIKI KATIKA FURAHA YA MUNGU YENYEWE

David Wilkerson (1931-2011)

"Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana" (1 Yohana 4:11). Upendo wa kila mmoja ulioelezwa hapa sio tu kushikana mkono, kumkumbatia haraka awo wakusifiana. Apana, aina hii ya upendo inaona haja ya mwingine na hufanya kitu juu yake. Kwa kweli, kulingana na Yohana, ikiwa tunamwona ndugu yetu akihitaji na tusifanye chochote, upendo wa Mungu hauko ndani yetu.

"Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli" (1 Yohana 3:18). Kwa wazi, kupendana hupendeza Mungu, lakini haiwezekani kupenda wengine mpaka utakapokubaliwa kikamilifu na upendo wa Mungu kwa ajili yako. Yohana anaandika, "Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake" (4:16). Hatuwezi kuwapenda wengine mpaka ukweli huu umesimama ndani yetu: "Licha ya udhaifu wangu wote na kushindwa, Mungu ananipenda!" Ikiwa una uhakika wa upendo wa Mungu kwako, upendo wake utamwagika kutoka kwako kwa kama kawaida.

Ikiwa tunashikilia chuki dhidi ya ndugu au dada, hatuna upendo wa Mungu. Zaidi ya hayo, ikiwa tunachomoa msamaha kutoka kwa mwingine, na Mungu atachomoa msamaha wake kutoka kwetu. Kwa hiyo upendo sio kitu tu cha kuongea. Ni suala la kufanya, kutenda, na kuishi.

Ikiwa unataka kumpendeza Mungu, Bwana atafungua macho yako kwa mahitaji ya wale walio karibu nawe. Wakristo wa Kiburi hawajui aina hii ya upendo kwa wengine. Zawadi ya kujali hutolewa tu kwa wale wanaoitafuta na kuomba. Roho wa Kristo atawajulisha mahitaji ya wengine, na kukufanya ulie, "Ndugu, dada, acha nisaidie. Ninataka kusimama na wewe wakati huu mgumu. "Mungu atakutumia mtu mmoja baada ya mwingine katika mahitaji - lakini haitakuwa mzigo. Badala yake, itakuvutia kwa sababu utashiriki katika furaha ya Mungu mwenyewe!