KUSHINDWA KUONA DHAMBI YETU WENYEWE

David Wilkerson (1931-2011)

"Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika [Yesu] ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Mfarisayo, akaketi chakulani. Na tazama, mwanamke mjini aliyekuwa mwenye dhambi, alipojua kwamba Yesu ameketi mezani ndani ya nyumba ya Mfarisayo. Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Mfarisayo, alileta chupa ya marimari yenye harufu nzuri. Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akila, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa miguu kwa nyele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale mafuta yenye harufu nzuri" (Luka 7:36-38).

Simoni, Mfarisayo huyu, alialika pia kundi lililochaguliwa la viongozi wa kidini kushiliki na meza ya chakula cha jioni. Ilikuwa ni wazi mkusanyiko wa kidini, uliofanywa na wanaume ambao wanajitapa wenyewe kuwa watu watakatifu katika kizazi chao. Kisha "mwanamke wa jiji" alijitokeza eneo hilo na akainama mbele ya miguu ya Yesu. Alikosha miguu yake yenye kuwa na vumbi kwa kutumia machozi yake na kuipangusha safi kwa kutimia nywele zake - kitu kilichokuwa sio cha kawaida kwa mwanamke mwenye heshima wa siku hiyo angeweza kufanya kwa umma. Hatimaye, alifungua chupa la mafuta yenye bei kali, na akamwagia mafuta hayo kwenye miguu ya Yesu.

Mafarisayo wakasirika, wakifikiri, "Ni aibu! Ikiwa Yesu alikuwa nabii wa kweli aliyetumwa kutoka kwa Mungu, angejua kwamba mwanamke huyu ni mwovu na kumzuia. "Hakika, Maandiko yanasema wale walikuwa mawazo halisi kama ya Simoni (angalia Luka 7:39). Yesu alisoma mawazo yake na kumtangaza, "Simoni, nina kitu kimoja nataka kukuambia" (7:40). Yesu aliwaambia hadithi ya wenye kuwa na madeni wawili, mmoja aliye na deni kubwa na mwngine aliyekuwa na deni kidogo, ambao walikuwa wamsamehewa na kuwa uhuru kutoka kwa mkopo wao. Kisha Bwana akaonyesha majitapo ya Simoni, roho ya hukumu na ukosefu wa huruma. "Simoni, huoni uharibifu wa moyo wako mwenyewe. Unamhukumu mwanamke alietubu, lakini ulishindwa kutambua kwamba unahitaji msamaa zaidi, au huruma zaidi."

Yesu alionyesha roho ya msamaha na kurejeshwa katika nyumba ya Mfarisayo usiku ule alipomgeukia mwanamke na kusema, "Umesamehewa dhambi zako" (7:48). Alikuja kuwa rafiki na kurejesha walioanguka, wasio na marafiki, wale waliopatwa na dhambi, na anatuambia leo, "Hii ndiyo huduma yangu yote. Hebu acha nipanue moyo wako kwa kuelekeza kwa wanao umizwa, watu waliovunjika ili uweze kupanua rehema yangu kwao."