KUSHINDA UVIVU

David Wilkerson (1931-2011)

Kama Marekani inapoingia zaidi katika uasi, watu wengi zaidi na zaidi wanataka kwenda njia yao wenyewe. Watu hawa hawataki kuvalishwa na Kristo mavazi ya samani kubwa ya haki; wanataka tu kuishi kwao wenyewe, bila yajibu au ahadi. Kwa mtazamo wao, wanamwambia Bwana, "Napenda kufurahia uhusiano wangu na wewe tu ili wengine wanione vizuri."

Makanisa ya Marekani na duniani yote yanajaa mamilioni ya watu wanaoitwa Wakristo ambao hawana urafiki na Yesu. Hawatumii wakati katika maombi na hawataki kuchukua Biblia zao ili wawone kile anachotaka kutoka kwao.

Kwa namna fulani, watu hawa wamejiunga na jina la Kristo kabisa kwa wao wenyewe. Bwana wetu hana sehemu katika hayo. Kristo anaonya waziwazi katika Marko: "Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba kwamba ni jioni, au kwaba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, naawambia wote, kesheni!" (Marko 13:35-37).

Tunasoma mfano wa mabikira kumi, watanu walikuwa wenye busara, na watano wapumbavu (tazama Mathayo 25:1-13). "Wakati bwana harusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi" (Mathayo 25:5). Wasichana wote, wote wajinga na wenye busara, walikuwa wamelala. Namuna gani hawa wasichana wenye hekima wangeweza kulala? Je, namna gani mtumishi wowote wa Mungu, wale ambao wamejiandaa kwa kurudi kwa Yesu kwa muda mrefu, wamelala wakati Bwana anakaribia?

Hebu tuangalie onyo la Paulo: "Kwamba saa ya kuamuka kutoka katika usingizi imekwisha kuwadia; usingizi; kwa maana sasa uokovu wetu u karibu kuliko tulipoanza kuamini" (Warumi 13:11). Paulo pia anawaambia, "Amka, wewe usinziaye, ufufuke katika wafu, na Kristo atakuangazia. Basi anagalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio nahekim bali kama watu wenye hekima; mkukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu" (Waefeso 5:14-16).

Ukijisikia kwamba uko mwenye uvivu kwa kumufuata Yesu, fikilia kwa kuangalia Yeye kwa roho yako yote, mawazo yako yote nafusi yako na nguvu zako zote. Anza kuomba kila siku na kumfanya Kristo awe katikati ya mawazo ya maisha yako.