KUSHINDA MBEGU ZA MASHAKA

David Wilkerson (1931-2011)

Yohana Mbatizaji alikuwa mtu wa Neno. Alitumia maisha yake yote akijifunza maandiko mahari pa upeke na kutafakari juu ya sheria. Alimwambia Yesu na kusema, "Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu" (Yohana 1:29). Alimwona Roho Mtakatifu akishuka juu ya Kristo kama njiwa, na akasikia sauti ya Baba ikumtangaza Yesu kuwa Mwana wake wa kipekee. Hata hivyo, Yohana alijikuta gerezani, huduma yake yenye nguvu, iliyotiwa mafuta imefupishwa na Mfalme Mwovu Herode (ona Luka 3:19-20). Sasa umati wa watu ambao ulikuwa unamfuata Yohana ulikuwa wakaondoka - "sauti ya mtu inayolilia jangwani" ikasimama.

Utumishi wa umma wa Yohana ulikuwa umekoma mwaka mmoja tu, lakini wakati huo, Mungu alikuwa ameonyesha uwezo wake kupitia mahubiri ya Yohana. Yesu alijua kwamba nabii huyo mwenye moto atakuwa amekufa kuliko kuendelea kufungwa gerezani. Baada ya yote, alikuwa ameishi miaka yake yote jangwani tupu, akitembea kupitia nchi na kulala katika mapango.

Wakati Yohana alipokuwa amefungwa, aina fulani ya jaribio la kina, giza la nafsi lilimtia na kuanza kushangaa. Yohana lazima alijiuliza kwa nini Yesu hakumtoa kutoka gerezani. Baada ya yote, Isaya alikuwa ametabiri kwamba Masihi angewaweka huru wafungwa wakati atapokuja. Kwa kweli, Yesu hakuishi kulingana na matarajio ya Yohana. Je! Yeye ndiye Masihi aliyeahidiwa? (Ona Mathayo 11:2-3.)

Ibilisi yule ambaye alijaribu Yesu jangwani, alijaribu tena kuharibu imani ya Yohana. Na anatumia uongo huo huo, na udanganyifu dhidi yetu leo. Lengo lake ni kupanda mbegu za mashaka ndani yetu kuhusu Neno la Mungu, ahadi zake, furaha yake ndani yetu. Shetani anataka usiwe na subira unaposubiri majibu ya maombi yako. Lakini kutokuwanaumanifu kwa Mungu kunaweza kusababisha maombi yako kuwa "harufu mbaya" badala ya kuwa harufu nzuri.

Yakobo 1:2-4 anatupa faraja hii: "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali, mkijua kwamba kujaribiwa kwa imani yenu huleta subira. Lakini uvumilivu uwe na kazi yake kamili, ili muwe wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa na neno."