KUSHIKAMANA NA YESU KWA MOYO WAKO WOTE

Gary Wilkerson

"Basi petro na Yohana walikuwa wakienda pamoja kwanda hekaluni, saa ya kuomba, saa tisa. Na mtu mmoja alieyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye ... ili aombe sadaka ... Lakini Petro akasema, "Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Simama uende ... na mara moja [miguu ya mtu] na nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Na akainuka upesi, akasimama na kuanza kutembea" (Matendo 3:1-2, 6-8).

Petro na Yohana walikuwa wamekwisha kujazwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, na walikuwa wanaona miujiza zaidi kuliko hapo awali.

Siku moja walipokwenda kwenye hekalu kuomba, walikutana na mtu mlemavu kwenye lango lililoitwa Mzuri. Walikuwa wamemwona mtu mara nyingi kabla lakini wakati huu alipoomba msaada, wakasema, "Tuangalie." Mtu huyo alidhani wanakwenda kumpa fedha lakini badala yake walimwamuru aende na kutembea - kwa jina ya Yesu. Mtu huyo alipokwenda na kuanza kutembea, wote ambao waliiona walikuwa wamejaa mshangao na wakaanza kumsifu Mungu.

Ni utukufu gani wa uzuli uliofuata kama watu wakishuhudia utukufu wa Mungu ukitenda kazi. Walikuwa na hofu na wakakusanyika ili kujadili kile walichokuwa wameona. Biblia inasema kwamba yule mtu aliyeponywa "aliwashika Petro na Yohana" (ona 3:11). Moyo wake ulipiga na alikuwa akisema, "Sitakuacha kurudi kwa uwepo huu wa ajabu wa Mungu."

Kila mwamini anapaswa kulia, "Bwana, unionyeshe utukufu wako. Ninakubali kazi yako ya ajabu, Mungu. Siridhiki na sehemu ndogo - Nataka utimilifu wa utukufu wako katika maisha yangu na nitashika Neno. Baba, nataka yote kutoka kwako. "Baba anapenda moyo unaomtafuta - na wakati anafanya kazi kubwa katika wewe, mshike kwa moyo wako wote!