KUPENDANA KWA UJASILI KAMA YESU ALIVYOFANYA

Gary Wilkerson

Tunapochunguza maisha yetu kama wafuasi wa Yesu, wengi wetu hafwaati mfano wa Agano Jipya. Kristo aliwatuma wanafunzi wake kumi na wawili kuitangaza habari njema, kuponya wagonjwa, na kuwa tayari vyombo vya kuleta ufalme wake duniani (angalia Marko 16:15-18). Baadaye, aliwatuma wanafunzi sabini na maagizo sawa (angalia Luka 10:1-16). Aliwaambia kila mmoja wa makundi haya, "Kila kitu niliowafundisha kufanya - kuhubiri injili, kuponya wagonjwa na kuleta ndani ya ufalme wangu - munapaswa kufanya hayo kwa jina langu. Sasa nenda ulimwenguni pote na mufanye kama nilivyoamuru."

Hiyo ni mfano wa Agano Jipya. Lakini pengo kati yake na njia tunayoishi imani yetu ni kubwa. Mwisho mmoja ni nguvu ya ajabu ya kazi ya Mungu, na kwa upande mwingine ni maisha yetu. Nini kinatuzuia kufanya kazi za Yesu? Ninaamini ni hii: tunahitaji ubatizo wa upendo wake.

Kikwazo kimoja zaidi kuliko chochote kingine kinachotuzuia kupenda kwa ujasiri kama Yesu alivyofanya. Kikwazo hiki ni hofu! Tunapofikiria kufanya kazi za Yesu, tunaogopa watu, wa kile wanachoweza kufikiri, na kushindwa. Mtume Yohana anasema hivi kwa moja kwa moja: "Hakuna hofu katika upendo, lakini upendo kamili hutoa hofu. Kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika upendo" (1 Yohana 4:18).

Paulo anaelezea zawadi ambazo hutolewa kutokana na kuwa huru kutoka kwa hofu: "Kwa maana Mungu hakutupa roho ya hofu, bali ya nguvu na upendo na moyo mzuri" (2 Timotheo 1:7). Hakuna katika uwezo wetu wa kibinadamu unaweza kutujaza na roho ya nguvu na upendo na akili nzuri. Hizi ni zawadi za Mungu, na anawapa wote wanaoziomba. Wakati atatuacha kutoka kwenye hofu, tunaweza kupenda watu tukiwa na upendo wake na kuwatumikia kwa mahitaji yao ya kina. Upendo wake hubadilisha kila kitu!