KUMTAMBUA YESU KATIKA DHORUBA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu aliwaagiza wanafunzi wake ndani ya mashua ambayo ilikuwa inaenda kugonga. Biblia inasema, "Yesu akawalazimisha wanafunzi wake kupanda mashua" (Mathayo 14:22) - ambayo ilikuwa inaenda ku kumbana na maji yenye mawimbi makali. Ilikuwa inaelekeya kutupwa kama ndege inayozama chini ya maji, na Yesu alikuwa alisha jua hayo yote kote kabla.

Yesu alikuwa wapi? Juu ya milima inayoonekana kwenye bahari hiyo, kuomba kwa wanafunzi kuwa wasingeweza kushindwa mtihani ambao alijuwa kwamba wangepaswa kupitia. Safari ya mashua, dhoruba, mawimbi ya kutisha, upepo wote, hayo yote yalikuwa ni sehemu ya majaribio ambayo Baba alikuwa amepanga. Wanafunzi walikuwa wanataka kujifunza kuhusu somo kubwa zaidi ambalo hawajawahi kujifunza: jinsi ya kumtambua Yesu katika dhoruba.

Juu ya jambo hili, walimtambua Yesu kama mtenda miujiza, Mtu ambaye aligeuza tupande twa mikate na samaki kuwa chakula cha muujiza. Wao walimtambua kuwa rafiki wa watenda zambi na musaidizi wa mahitaji yao. Hata walimtambua kuwa Mwana wa Mungu na yule ambaye aliewafundisha jinsi ya kuomba, kusamehe, na kufunga na kufunguwa. Lakini kwakeli wale ambao walidhani kwamba wanamjua Yesu vizuri sana, hawakumtambua wakati dhoruba ilipopiga.

Hiyo ndiyo mizizi ya matatizo mengi leo. Tunamwamini Yesu kwa ajili ya miujiza, tunamwamini kwa ajili ya wokovu wetu, na kumtazamia ili atupatiye mahitaji yetu, lakini wakati inaonekana kama kila kitu kinaangukiya kando, hatuwezi kamwe kuwa kimya kwa kuwa na uhakika kama yuko karibu.

"Boti lilikuwa katikati ya bahari, likipigwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa mkali. Sasa katika saa ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akitembea kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akitembea juu ya bahari, wakawa na wasiwasi, wakisema, "Ni pepo!" Wakalalamika kwa hofu" (Mathayo 14:24-26). Hii ni hatari ambayo sisi sote tunakabiliwa na – kwakutoweza kumwona Yesu katika shida zetu.

Yesu daima anatukaribia kwetu kwa kujifunua yeye mwenyewe kama Mwokozi katika dhoruba. Anakutaka wewe umutumaini katika kila dhoruba ya maisha yako. Huyo ndio uwepo wa Yesu unavyomanisha wote!