KUMKARIBIA MUNGU KATIKA MAOMBI

David Wilkerson (1931-2011)

"Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;  kwa maana mtu amwendeaye  Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba yeye huwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii" (Waebrania 11:6).

Mara nyingi tunasikia mafundisho kuhusu jinsi tunapaswa kuja mbele ya Mungu kwa imani, lakini kuna mambo ambayo mtu hafai kufanya wakati unakuja kwake kwa maombi. Kwa mfano, fusimwendee Mungu ukimtarajia afanye jambo lolote jema isipokuwa ukija na imani kama ya watoto katika ahadi zake. Neno la Mungu liko wazi: "Ila aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote, maana mwenye kuwa na shaka ni kama wimbi la bahari inayoongozwa na upepo" (Yakobo 1:6).

Wapenzi, haiwezekani kwako kumpendeza Mungu bila imani! Ibrahimu alikuwa mtu ambaye alikua na imani ambayo haishanguki kwa yale ambayo Mungu alimwahidi: "Na yeye hakukuwa dhaifu katika imani ... Lakini akiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutoamini, lakini alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale alioahidi” (Warumi 4:19-21).

Usimwendee Mungu na aina yoyote mashiriti. Ahadi yoyote ya Mungu ni ufunuo kuhusu mapenzi yake. Kwa mfano, chukua ahadi ya Mungu ya "yule awezaye kuwalinda ninyi msijikwaze, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila lawama mbele za uwepo wa utukufu wake kwa furaha tele" (Yuda 24). Hautamuuliza Mungu ikiwa ni mapenzi yake kukuzuia kuanguka wakati tayari amekwisha ahidi kulifanya. Kwa kweli, Mungu hutupa ahadi kubwa na za thamani ili tujifunze kumwamini kwa ujasiri: "Basi na tukikaribie kwa ujasiri kiti cha neema, ili tuipate neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" (Waebrania 4:16).

Usimwendee Mungu hadi pale uko tayari kuamini kwa kile unachoomba. "Yoyote munaombayo mukiomba, amini ya kwamba munayapokea, na mutayapata" (Marko 11:24). Ikiwa utamwomba Mungu mkate, hatakupa jiwe. Ukimuomba samaki, hatakupa nyoka (ona Mathayo 7:9-10).

Muamini Mungu kwa hali yako ya kimwili, hali yako ya kifedha, familia yako, ukuaji wako wa kiroho. Linganisha ahadi zake - zote ni zako! Amina!

Tags