KULINDWA KUTOKA KUANGUKIA NJE

David Wilkerson (1931-2011)

Mtume Paulo anazungumzia uasi mkubwa unaokuja duniani katika siku za mwisho. Je, uasi ni nini? Ni "kukataa ukweli ilioaminiwa na kutangazwa."Kwa ufupi, ni kuangukia mbali na ukweli wa Mungu. Paulo anaandika juu ya uasi unaokuja: "Basi, ndugu, tunakusii kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno ... kwamba siku ya Kristo imekwisha kufika. Mtu yeyote asiwadanganye kwa njia yoyote; kwa maana Siku hiyo haitakuja isipokuwa kuanguka ndio kukuja kwanza" (2 Wathesalonike 2:1-3).

Baba zetu wa kiroho katika kanisa la Agano Jipya walikuwa watumishi ambao walitoa maisha yao kwa kuyilinda injili. Kutoka mwanzo, wanafunzi na mitume walihubiri mashauri yote kutoka kwa Mungu, wakimtangaza Kristo kama Masihi kwenye siku zao za kufa. Bwana alimimina zawadi na baraka zake juu yao na kanisa lilikua linafanikiwa katika roho na kwa kweli.

Kati ya mizizi ya kanisa hilo la kwanza lilipanda mti na matawi mengi tunayoiita miundo, madhehebu, mashirika, ushirika - kama Wabatisti, Methodisti, Presbyterian, Lutheran, Wapentekoste, Episcopaliana na wengine. Wengi wa matawi haya yalikuwa moto kwa watumishi watakatifu wa Kristo, ambao baadhi yao waliuawa kwa kujitolea kwa Neno la Mungu lilio safi.

Mungu huchukia injili isiokuwa joto au baridi kwa kuwa nusu ya ukweli ambayo sasa inaenea duniani kote. Yesu alikuja ulimwenguni ambao ulikuwa katika uasi wa jumla, na kuja kwake kulikuwa ni tendo safi la huruma, lisilopendezwa kwa mtu yeyote. Mavuno mazuri ya roho bado yanakuja katika umri huu wa kisasa na waumini wenye njaa kutoka kila taifa watatambua sauti ya Bwana. Mioyo yao iliyoamka itasema, "Bwana, narudi kwenye upendo wangu wa kwanza kwa ajili yako."

Ikiwa umetembea na Mwalimu kwa muda mrefu, huenda unahitaji mtu wa kukumbusha kumkaribia na kupata upya upendo wake wa kwanza, usije "kuanguka" na kuwa sehemu ya uasi mkubwa huu. Mpendwa, anakusubiri kukumbatia na kukupeleka kwenye mahali mapya pamoja naye.