KUKUMBUKA HURUMA YA YESU

David Wilkerson (1931-2011)

Inawezekana kusema, "Ninaamini Mungu anaweza kufanya jambo lisilowezekana," na tena unakuwa hauwezi kukubali miujiza ya Bwana kwa ajili yetu wenyewe kwa sababu ya moyo yenye kuwa na mashaka. Katika Mathayo tunaona Yesu akiingia ndani ya mashua akaenda "mahali pasipo watu" (14:13). Alikuwa amekwisha kupokea neno ambalo Yohana Mbatizaji kama alikuwa amekatwa kichwa, na alivutiwa sana na habari kwamba alihisi haja ya kuwa peke yake ili aomba. Hata hivyo, watu waliposikia kwamba Yesu alikuwa anaondoka, "wakamfuata kwa miguu kutoka mijini" (aya hiyo).

Maelfu ya watu alikuja akitoka pande zote katika aina zote za hali ya kimwili. Walemavu walichukuliwa juu ya watetezi au magurudumu kuelekea kwake katika mikokote yenye kuwa na nyumba. Wanaume kwa wanawake wenye kuwa vipofu waliongozwa kupitia umati wa watu, na walemavu walijitokeza kenda mbele wakiwa kwenye vitu vyakuwasayidia kutembea. Wote walikuwa na lengo moja lililokuwa linaloendelea: la kuwa karibu na Yesu na kupokeya uponyaji!

Na ni majibu gani kutoka kwa Kristo kwenye hali hiyi ya ajabu? "Akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao" (Mathayo 14:14). Kisha, mwishoni mwa siku hiyo ya ajabu na baada ya kufanya miujiza yote ya uponyaji, Yesu aliamua kulisha umati mkubwa (ona Mathayo 14:16-21).

Baadaye, kwenye mashua kuelekea Magdala, wanafunzi walikuwa wamechoka kutokana na kutumika siku nzima na wakaanza kuzozana kwa sababu walikuwa na mkate mmoja kati yao (tazama Marko 8:14). Fikiria! Petro, Yakobo, Yohana na wengine walikuwa na wasiwasi juu ya mkate wakati walikuwa wamemaliza kutoka kwenye malisho makubwa zaidi katika historia! Yesu hakuamini hayo na akawakemea, "Je! Hamjafahamu bado?" (8:21).

Ujumbe huu ni kwa wote walio kwenye ukingo wa uchovu, wewe mwenye kuzidiwa na hali yako ya sasa. Umekuwa mtumishi mwaminifu, ukiwalisha wengine chakula, ukiamini kuwa Mungu anaweza kufanya mambo yasiyowezekana kwa watu wake, lakini unashikilia kuwa na mashaka juu ya nia yake ya kuingilia kati katika mapambano yako mwenyewe.

Roho Mtakatifu anakuita kukumbuka huruma ya Yesu, kumbuka gisi alifanya mikate na samaki kuwa vingi, na ujue kwamba hataki hata mmoja wenu akate tamaa.