KUKATAA KUWA KIMYA KATIKA SALA

Carter Conlon

Endelea kuwa na nguvu wakati Mungu anaonekana kuwa kimya, kwa kuwa ushindi bado ni wako. Haijaondolewa kutoka kwako; haujatemwa kutoka kwa uzima wa Mungu kwa sababu ya makosa machache unakumbana nayo katika safari, kwa hilo sivyo Mungu anavyofanya. Erekeya tu kwake kama mfalme Daudi alivyofanya - kwa moyo wako wote.

Baada ya kupitia wakati wa kuwa kimya - kwa shida, giza na machafuko - Daudi aliandika maneno haya kama sehemu ya kujitolea kwa hekalu: "Bwana, kwa radhi yakow ewe uliumarisha mlima wangu. Uliuficha uso wako, name nikafadhaika. Ee Bwana, nalikulilia wewe, naam, kwa Bwana niliomba dua" (Zaburi 30:7-8). Daudi alikuwa anasema, "Kulikuwa na msimu katika maisha yangu ambapo ulificha uso wako kutoka kwangu. Ilionekana kuwa hakuwapo tena. Katika asili, yote niliyoyaona ilikuwa uharibifu ulionizunguka, upumbavu wa makosa yangu mwenyewe. Ilinifanya kuwa na wasiwasi, lakini nilikulia wewe."

"Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; ulinivua gunia, ukanivika furaha. Ili utukufu wangu ukusifu, wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, nitakushukuru milele" (30:11-12). Kwa maneno mengine, "Hata wakati mimi ni mpumbavu, unabaki mwaminifu. Umeweka wimbo wa sifa ndani yangu ambayo inategemea hali yangu. Umeweka imani ndani ya moyo wangu ili mambo yawe sawasawa na wewe ulivyosema, kwa kuwa itakuwa hivyo nitaimba sifa na kutowa shukrani."

Kwa njia hiyo hiyo, Mungu tayari ameweka wimbo ndani ya moyo wako. Hata ingawa anaonekana kimya kwako, kataa kuwa kimya. Furahia ndani yake, ukijua kwamba hakika atatimiza ahadi zote alizowapa. Mungu amekuwa mwaminifu kwako na atakuwa mwaminifu daima!

Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji muanzilishi, David Wilkerson, na alichaguliwa kuwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.