KUKAA NDANI YA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu atakuacha lini kukupenda? Atasimama tu ikiwa anaacha Mwana wake mwenyewe, ambayo haiwezekani. Kristo anasema, "Naye aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo" (Yohana 13:1). Hii inatusaidia kuelewa vizuri zaidi kile Yuda anachosema wakati anapofundisha, "Jilindeni katika upendo wa Mungu" (Yuda mstari wa 21). Anatuambia, "Weka ukweli huu, ushikilie na usuiache kamwe. Kujua upendo wa Mungu kuna maana ya faraja yako, nguvu yako. Itakufanya kuwa huru na kukuweka kuwa huru.

Kujiweka katika upendo wa Mungu ni kujua, kuamini na kuendelea kutegemea upendo wake hata katika shida zako.

Yohana anatuambia jinsi tunaweza kujiweka katika upendo wa Mungu: "Nasi tumelifahamu tendo alilo nalo Mungu kwetu sisi,na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake" (1 Yohana 4:16, Biblia ya Mfalme Yakobo (KJV). Kwa kifupi, ikiwa "tunakaa katika upendo wa Mungu," tutajiweka katika upendo wake.

Neno "kukaa" linamaanisha "kubaki katika hali ya matarajio.” Kwa kifupi, Mungu anatutaka tutalajiie upendo wake kuwa upya kwetu kila siku. Tunaombwa kuishi kila siku ndani ya ujuzi kwamba Mungu ametupenda kila wakati na ataendelea kutupenda kila wakati.

Anatuambia katika vifungu hivi, "Bila kujali jaribio gani unalokabiliana nalo, usiwe nashaka kamwe kwa upendo wangu kwako. Kama unategemea kikamilifu katika upendo wangu, basi unaishi kwa njia ambayo nataka uishi.”

Je, unaendele kuishi ndani ya majaribu makubwa? Je, umeshindwa na tamaa ya zamani ambazo unachukia? Je! Ndoa yako inafadhaika, familia yako iko katika machafuko? Hizi ndiyo nyakati unazohitaji ili ujiweke ndani ya upendo wa Mungu. Unapaswa kujua kwamba, japokua unapitia hayo yote, Baba wa milele bado anaendelea kukupenda sana.