KUJILINDA DHIDI YA KURUDI NYUMA KUTOKA KWA KRISTO

David Wilkerson (1931-2011)

Inawezekana kwa Wakristo kuwa wanazarawu mambo ya kiroho, kushikiliwa nakutokuomba, kupitia siku yote bila kutafuta Neno la Mungu. Naam, Biblia inaonya kwa wazi kwamba inawezekana kwa waumini wenye kujitolea kujitowa kwa Kristo na inatoa maonyo yenye nguvu juu ya kujilinda usingizi katika saa ya usiku wa manane: "Kwa hiyo imetupasa kuyaangilia zaidi ya hayo yaliosikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii?" (Waebrania 2:1-3).

Kuna mifano ya kibiblia ya makanisa ya mara moja yenye nguvu ambayo yalimalizikia kwa kurudi nyuma. Katika Ufunuo, tunasoma juu ya kanisa la Efeso likiumiza Kristo kwa kujiweka mbali na upendo wao wa kwanza (Ufunuo 2:4). Vilevile, kanisa la Laodikia liliporudi nyuma kwa kujiweka katika hali ya joto (3:15), na kanisa la Sarde likageuka kifo cha kiroho (3:2). Paulo anawaonya waumini wa Galatia kwamba walikuwa wamepotea kutoka ushindi wa msalaba wa Kristo na walikuwa wamegeuka nyuma kwa kazi za mwili (tazama Wagalatia 1:6-7).

Paulo anaonya hivi, "Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima" (Waefeso 5:15).

Unawezaje kujilinda dhidi ya kuludi nyuma kutoka kwa Kristo na kukataa "wokovu mkubwa"? Paulo anatuambia "tujali" kwa mambo tuliyoyasikia. Kusoma kasi kwa njia ya Neno la Mungu kunaweza kuwa na hisia moja ya kufanikiwa, lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba "kusikia" yale unayosoma na masikio ya kiroho. Fikiria juu ya Neno ili ulisikie moyoni mwako.

Paulo anasema, "Jitathmini wenyewe kwamba mmekuwa katika imani. Jaribu mwenyewe. Je, hamjui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu?" (2 Wakorintho 13:5). Anawahimiza, "Kama wapenzi wa Kristo, jijaribuni mwenyewe; chukua muda wakufanya hesabu ya kiroho ya kutembea kwako na Yesu." Ninakuhimiza kufanya hivyo. Jinsi ya ushirika wako na Kristo? Je, unalinda kwa bidii yote?