KUGEUZWA NDANI YA SURA YAKE

David Wilkerson (1931-2011)

Maandiko yanaonyesha kuwa inawezekana kwa kila mfuasi wa kweli wa Yesu kuona na kuelewa utukufu wa Mungu. Hakika, Bwana wetu anafunua utukufu wake kwa wote wanaouomba na kuutaka kwa bidii. Naamini ufunuo wa utukufu wa Mungu utawawezesha watu wake kuvumilia siku zenye hatari.

Utukufu wa Mungu sio udhihirisho wa kimwili au hisia ya furaha ambayo inakushinda. Wala sio aina isiyo ya kawaida au mwanga wa malaika ambao hupasuka. Weka tu, utukufu wa Mungu ni ufunuo wa asili na sifa zake!

Tunapoomba, "Bwana, unionyeshe utukufu wako," tunaomba kwa kweli, "Baba, unifunulie mimi nijuwe wewe ninani." Bwana anataka kutufunulia jinsi anataka kujulikana. Bwana alimtuma Musa kuwaokoa Israeli bila kumpa ufunuo kamili wa nani Mungu wa Israeli alikuwa. Bwana alimwambia, "Nenda, na useme MIMI NIKO amenituma" Lakini hakuwa na ufafanuzi kuhusu nani "MIMI NIKO" alikuwa.

Naamini hii ndiyo sababu Musa alilia, "[Bwana], Nakuhisi, unionyeshe utukufu wako" (Kutoka 33:18). Musa alikuwa na njaa ya kutaka kujua mwenye nguvuni MIMI NIKO alikuwa ni nani - kujua maumbile na tabia vyake. Naye Bwana akajibu sala yake. Kwanza, alimufundisha Musa kujificha katika shida ya mwamba ambapo Mungu alikuja kwake kwa ufunuo rahisi - hakuna radi, umeme, au kutetemeka kwa dunia.

"Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana Mungu, mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi" (Kutoka 34:6-7) .

Mungu alimruhusu Musa kuona utukufu wake ili apate kubadilishwa na kuuona. Na hiyo ni kweli kwetu leo. Mungu hufunua utukufu wake kwetu ili, kwa kuuona, tunaweza kubadilishwa kuwa sanamu yake mwenyewe.