KUEPUKA MAISHA YA MAJUTO

Jim Cymbala

Ujasiri wa kiroho ni haja kubwa kwa wengi wetu leo. Tunaweza kusikia mafundisho bora na kusoma tafsiri nyingi za Biblia. Lakini tunachohitaji kufanya ni "kuchochea" kazi ya Roho ndani yetu. Tunapaswa kujitolea upya kwa Mungu kwa sala, kusoma Biblia, na kujitoa kwa Roho Mtakatifu. Tunapaswa pia kujitenga na mawazo, maneno, na matendo yanavyozuia mtiririko wa Roho. Andiko linasema, "Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi" (Yakobo 4:8).

Ikiwa sisi hukaribia kwa unyenyekevu kwa urafiki mpya na Mungu,Je! Atatuachia nje? Ikiwa yeye alitupa Yesu wakati tulikuwa bado wenye dhambi, je, sasa kama Baba yetu wa mbinguni atakataa maombi yetu kwa zaidi ya ujasiri wa Roho na bidi? Hiyo itakataa kila kitu tunachokijua juu yake kutoka kwa Maandiko!

Waumini wangapi wanakuja mwishoni mwa maisha yao na kujisikia kama kwa namna fulani walikosa utimilifu wa mpango wa Mungu kwa maisha yao? Wanafikiria kwamba labda Mungu alikuwa na kitu fulani kilichopangwa, lakini kilichokuta. Hii ni wazo ya kusikitisha. Lakini ikiwa tunaruhusu Roho kutembeya akipitia kwetu, tutaona mipango na malengo yake yametimia. Hatutakiwi kuja mwishoni mwa maisha yetu ya kutubu fursa nyingi zilizopotea za kutumika zaidi kwa ajili ya Kristo.

Wakati unapkuja utaamua ni jinsi gani tunavoruhusu Mungu Roho Mtakatifu kufanya kazi na kupitia kwetu. Tunaweza kuishi siku zetu nje kwa kuwa na hofu ya kusita kwa kutabili, au tunaweza "Acha twende na acha Mungu." Mpango wa Mungu kwa ajili yetu sio juu ya nani sisi na talanta gani tunayoleta kwenye meza. Ni juu ya rasilimali na neema Mungu ametuahidi.

Kwa hiyo tunasema kwa ujasiri, "Bwana ndiye msaidizi wangu; sitaogopa. Wanadamu wenzangu wanaweza kufanya nini kwangu?" (Waebrania 13:6, msisitizo aliongeza).

Jim Cymbala alianza Hema la Brooklyn (Brooklyn Tabernacle) akiwa na wanachama wasio zidi ishirini katika jengo la chini katika sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.