KIVULI CHA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Yeremia nabii asiye na hofu, mhubiri mwenye nguvu wa utakatifu na toba, alikuwa na akili ya Mungu na akutembeya katika hofu ya Bwana. Hata hivyo, tunaposoma Yeremia 20, tunamwona huyu mtu mukubwa anayesumbuliwa na kivuli cha imani.

Yeremia alikuwa akihubiri kwenye lango la hekalu ambapo kasisi wa kishetani, Pashuri, alitembeya na kujipiga makofi. Ndipo Pashuri akawaamuru watu wake kumfukuza Yeremia na kumfunga katika hisa za umma, ambako alikuwa anachambiwa na wapiti njia. Alipotolewa, Yeremia alitangaza hukumu ya Mungu juu ya Pashuri na wafuasi wake: "Na wewe, Pashuri, na watu wote wanaoishi katika nyumba yako, mtakwenda utumwani" (Yeremia 20:6). Kwa maneno mengine, "Pashuri, wewe na mji huu unashuka!"

Mara tu hili lilipotokea, giza la roho lilishuka kwa Yeremia na akaanguka katika kukata tamaa. Mhubiri ambaye  wakati mmoja aliingiwa na utakatifu  sasa anafungulia hisia za giza kuelekea kwa Mungu: "Ee Bwana, umenihadaa. Neno ulionipa limekuwa ni aibu na kila siku ninaposhwa. Umeniacha, kwa hiyo ninakukana. Sitaki kuzungumza Neno lako tena kwa sababu ahadi zako zote ni tupu. Maisha yangu na huduma yameishia kwa aibu. Ungelipaswa kuniuia tumboni" (angalia Yeremia 20:7-9, 17).

Je, Yeremia alivuka mstari hapa? Je! Lugha hiyo inaweza kutokea kwa mtu yeyote anayedai kumtumikia Mungu? Tunapata jibu letu katika sura inayofuata sana: "Neno hili ndilo lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana" (Yeremia 21:1). Kivuli cha imani ya nabii kilipita, na Mungu hakuhindwa kupiga. Yeye daima anajua vifaa na mashambulizi ambayo Shetani anatumia dhidi ya watumishi wake wenye ufanisi zaidi na alijua Yeremia angeweza kuvumilia. Mungu alielewa kwamba malalamiko ya Yeremia yalitoka katika machafuko na maumivu, na Maandiko yanaonyesha kuwa si kwa muda mmoja Mungu aliondosha upako wake kutoka kwake.

Huenda umehisi kwamba Mungu amekuacha. Jihadharini kwamba shetani yuko nyuma ya mashaka haya, na ameamua kabisa kuzuia maono yako ya huruma na neema ya Mungu. Lakini nenda kwa Baba yako na upumzike katika upendo wake pamoja na uhakika kwamba hakukuacha kamwe.