KILIO CHAKO HUSUKUMA MOYO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Neno la Mungu linashuhudia ukweli kwamba mateso hutufundisha kupiga magoti na kulia mbele ya Bwana katika shida zetu zote na matatizo yetu.

"Kabla sitajateswa mimi nilipotea, lakini sasa nimelitii neno lako" (Zaburi 119:67).

"Najua, hukumu zako ni za haki, Ee Bwana, na kwa uaminifu umenitesa" (119:75).

Katika mstari wa mwisho, Daudi anasema, "Bwana, najua kwa nini unaniumiza. Uliona kuwa wakati wote ulipokuwa ukienda vizuri, nilikwenda kinyume na kuwa na mashaka, hivyo ukaruhusu shida ikanijia. Ulilijua kwamba ingeniongoza kwa magoti yangu na kunirudisha nyuma kwa kushindwa kabisa. Dhiki yangu ilikuwa ushahidi wa uaminifu wako kwangu!"

Tunahitaji kuelewa kitu juu ya moyo wa Mungu - huumizwa wakati tunapoumizwa. Anahisi maumivu yetu pamoja na sisi, bila kujali ni nini. "Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokowa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale" (Isaya 63:9-10).

Bwana hutembelea kila wakati watoto wake wanamlilia kutoka kwa taabu. "[Israeli] alilia; na kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. Mungu akasikia kuugua kwao" (Kutoka 2:23-24). Kilio cha Israeli kilichochea moyo wa Mungu. Kila wakati waliteseka, Mungu aliumizwa pamoja nao. Biblia inatuambia kwamba hata wakati Waisraeli walipotenda zambi dhidi ya Bwana na taabu ikawa juu yao, "Na roho yake ilihuzunika kwa sababu ya msiba wa Israeli" (Waamuzi 10:16).

Watu wengi wanapigana na utumwa mbaya katika maisha yao na majaribu yao katika ghadhabu kila siku. Hata hivyo, nasema kwa watu wote, "Mungu hujali!" Naam, anajua shida unayopitia na yeye pekee ana uwezo wa kukuokoa. Katika vita vyote, yeye anafundisha kukimbilia msalabani na kumlilia kwa ajili ya ukombozi!