KAZI YA YESU

Gary Wilkerson

Andiko tunalolijua ambalo linaelezea kusudi la Yesu hapa duniani  linapatikana katika Luka 4:18-19: "Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa."

Popote Yesu alipokwenda, moyo wake ulikuwa unaguswa na mahitaji ya watu. Wakati wowote alipomwona mtu anahitaji kuponywa, alisimama na kuwaponya. Kwa kweli, angeondoka na kuendelea na njia yake, ikiwa ni lazima, kuwapata waliokuwa na mahitaji. Watu walipokuwa na njaa, Yesu aliwapa chakula. Alikuwa na huruma nyingi kwa  walioumia, walemavu, vipofu, wale waliokuwa kama kondoo bila mchungaji.

Yesu hakuwa mponyaji wa kutembea tembea, ingawa aliponya kila mahali alipokuwa akienda. Yeye hakuwa mtetezi wa kijamii wa kutembea tembea, ingawa alionyesha huruma. Kimsingi Yesu alikuwa mhubiri! "Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akihubiri Habari Njema ya Mungu" (Marko1:14). Alikuja kuwafungua mateka, kuhubiri habari njema za nguvu zake za kuokoa, kuwasilisha Injili.

Ikiwa kila mmoja wetu angeweza kupokea maono kama Yesu alivyokuanayo, kazi yake ya msingi juu ya uso wa dunia ingekuwa pia  lengo letu la msingi. Tungejawa sana na upendo wa Kristo hata kusiwe na la kutuzuia kuutangaza. Watu walio karibu nasi hawangeweza kuepuka jina la Yesu liliokuwa likitajwa kwao. Niamininisemapo maneno ni muhimu! Matendo ni mazuri, lakini hakuna utangazaji wa kweli wa injili bila maneno.

Usione haya kuongea kumhusu Yesu. Mruhusu Roho Mtakatifu akuwezeshe hivi kwamba maneno yatakutoka kama jambo la kawaida. Yesu anataka sisi tutumie injili kwa kuwasilisha ukweli na maisha kwa wengine.