KABLA YA KUUMBWA, MUNGU ALIKUWA ANAKUJUA

David Wilkerson (1931-2011)

Kulingana na Yesu, kwa macho ya Mungu Kristo na Kanisa lake ni moja. Paulo anaonyesha hili kwa mfano wa mwili wa mwanadamu. Anasema Kristo ndiye kichwa na sisi ni mwili wake - mfupa wa mfupa wake, nyama ya mwili wake. "[Mungu] akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa, amabalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote" (Waefeso 1:22-23). "Kwa maana sisi ni viungo vya mwili wake, wa mwili wake na mifupa Yake" (Waefeso 5:30).

Maana hapa ni kwamba wakati Baba alimpenda Yesu mbele milele na milele, yeye alitupenda, pia. Hakika, wakati mtu alikuwa bado mawazo tu katika akili ya milele ya Mungu, Bwana alikuwa tayari akihesabu idadi yetu na kupanga mipango yetu ya ukombozi: "Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo" (Waefeso 1:4).

Katika Zaburi, Daudi anaandika kwamba alipendwa na Mungu wakati akiwa tumboni. "Naam, wewe ndiwe uliyenitoa tumboni,  ulinitumainisha matitini mwa mama yangu. Kwako nalitupwa tangu tumboni, toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu" (Zaburi 22:9-10).

"Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado" (Zaburi 139:16). Kwa kweli, Daudi anasema, "Hata kabla ya kuumbwa, unanijua, Bwana. Ulikuwa na sehemu zangu zote zilizowekwa chini kabla."

Mungu alikupenda kabla ya ulimwengu kuanza na hakuna mwisho wa upendo huo. "Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake" (1 Yohana 4:16). Ikiwa tunakaa ndani ya Mungu, tunaweza kutarajia upendo wake kuwa mupya kwetu kila siku. Angalia mawazo haya ya ajabu! Hata wakati wewe uko katika shida ya aina fulani, unaweza kujua kwamba kwa njia yoyote, Baba bado anakupenda.