JE, UMECHOKA NA JITIHADA ZAKO MWENYEWE?

Gary Wilkerson

"Kwa hiyo, muandaeni akili zenu kwa kutenda, na kuwa wenye akili, mkitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wa Yesu Kristo ... lakini kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi pia muwe watakatifu katika mwenendo wenu wote, kwa maana imeandikwa, 'Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu'" (1 Petro 1:13-16).

Unaweza kujisikia kama kwamba umechoka kikamilifu kwa jitihada zako zote za kuwa mtakatifu. Umeshindwa mara nyingi, na hii ndiyo nafasi yako ya mwisho. Lakini Mungu haakuambii kuwa mtakatifu kwa namna yeye alivyo, kwa sababu kwa hakika wewe awuna umungu. Mungu hawezi kusema, "Nitazame na kujaribu jitihada zako kwa nguvu zako mwenyewe kuwa kama mimi." Hapana - na hii ni utukufu - anasema kwamba "utakuwa mtakatifu" kwa njia ile ile aliyotangaza, "Jua, kutowa mwanga angani. Dunia ikafanyika. Maji akamwagika juu ya Dunia." Kama vile vile aliyoumba mbingu na Dunia - kwa kuzungumza katika ya uwapo - ni ndivyo hivyo anavyozungumza utakatifu wako katika uwapo.

Mungu hakwambiye, "Hebu angalia jinsi unavyoweza kuwa mzuri." Sio kama hivyo kabisa. Anasema, "Natangaza kwamba utakuwa mtakatifu. Ninazungumzia katika uwepo kama wewe ni mtakatifu. Mimi nitakufanya wewe kuwa kama mimi. Nimekupa Neno langu linalobaki kuwa milele - na ni nguvu. Ni uhai! Ni furaha! Ni ushindi! Na ninaweka yote ndani yako."

Mungu hakualiki wewe kujaribu kuishi maisha ya utakatifu; yeye anasema maneno haya juu yako. Inaweza kuchukua muda na kunawezakana kuwa na dhoruba na vita vya kimwili, lakini utapitia utakaso polepole. Anakufanya kuwa mtakatifu! Hilo linapaswa kukujaza furaha na matumaini. Kuhimizwa na kuongozwa na ujasiri kamili kwamba Mungu ni kwa ajili yenu na sio dhidi yenu.