JE! TUNA SHAUKU YAKUWONA IMANI YETU INASAFISHWA?

David Wilkerson (1931-2011)

Wapenzi, Mungu anataka watu ambao wanamtegemea kikamilifu. Bwana hakutuokoa ili tuweze kuzunguka kwa kudumu katika wema wake, rehema na utukufu. Alikuwa na kusudi la milele katika kuchagua kila mmoja wetu na kusudi hilo linakwenda zaidi ya baraka, ushirika na ufunuo. Ukweli ni kwamba, Mungu bado anafikia wanadamu waliopotea, kutafuta watu wenye Imani, anaweza kubolesha kama chombo chake kikubwa cha uinjilisti.

Mungu alikuwa akiwatafuta watu hao katika siku za Gideoni. Gideoni alipotoa wito wa kujitolea kupigana na Wamidiani, maelfu ya Waisraeli walijibu. Lakini Bwana akamwambia Gideoni, "Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno kwa Mimi kuwatia wamidiani katika mikono yao ... tangaza habari masikioni mwawatu hawa, na kusema, 'Mtu yeyote anayeogopa na kutetemeka, arudi'" (Waamuzi 7:2-3).

Mungu alikuwa akiwaambia Gideoni, "Ikiwa mtu yeyote anaogopa, mwambie aende nyumbani sasa. Sitaruhusu jeshi langu kuambukizwa na hofu. "Mungu alikuwa akiwaacha inje wenye kujitolea kwa jeshi lake; wakati mmoja, wenye wasiwasi 22,000 waliludishwa nyumbani. Gideoni hatimaye alipunguza idadi ya waliojitolea kufikia 10,000 lakini Mungu alimwambia kama walikua bado ni wengi sana, na hatimaye Bwana aliweka askari 300 waliopigana vita.

Hii inapaswa kutuambia kitu fulani. Kama Bwana anataka wajumbe wa injili anaweza kutuma ulimwenguni, hataajiri makanisa ambayo hujazwa na watu wenye hofu, wasiwasi, wasioamini. Hatatafuta mashirika yenye nguvu, yenye ufanisi wa kidini au wenye kusoma elimu kubwa kutoka seminari. Mungu hutumia mashirika na wenye ujuzi, bila shaka, lakini kwao wenyewe hakuna hata mojawapo ya haya ambayo yanahitajika kuwa wajumbe wa Mungu waliojaribiwa.

Kwa hiyo, ni nini kinachohitajika ili kufikia ulimwengu uliopotea na unaoumizwa? Mungu anajitafutia wale ambao wanataka kupimwa, wanajaribiwa kwa moto, wale ambao imani yao inaweza kuifanya na kuzalisha kama dhahabu safi.