JE! MOYO WAKO HAUNA HATIA?

David Wilkerson (1931-2011)

"Ninyi ni mashuhuda, na Mungu pia, jinsi tulivyojitolea kwenu mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa" (1 Wathesalonike 2:10).

Paulo alikuwa mhubiri mzuri ambaye angeweza kusimama kwa ujasiri mbele ya watu na kushuhudia, "Wenzangu, mimi nimeishi maisha yasiyokuwa na hatia mbele yenu na mbele ya Mungu. Tabia yetu ilikuwa ya haki na safi. Ninatembea kila wakati kwa kuonekana kwamba macho yake yako juu yangu, na nyinyi pia muko mashahidi wa maisha yangu.” Alitaka kila mwamini awe na nguvu ile ile aliyokuwa nayo katika kuwaelekeza watu kwa Mungu kupitia kuishi maisha yasiyokuwa na hatia. Lakini mtu yeyote anawezaje kuishi bila hatia, na ni nini kinachoonesha maisha ya aina hiyo?

  1. Mkristo asiye na hatia ni mtu asiye na udanganyifu moyoni mwake. Paulo alisisitiza kwamba yeye hakuwa mudanganyifu, kwakuhubiri jambo moja, na kuishi lingine. Lakini pia alionya kuwa watu wengine walikuwa wanakwenda kudai kuwa mitume. "[Lakini] maana watu hao ni manabii wa uwongo, wafanyikazi wadanganyifu" (2 Wakorintho 11:13). Paulo alisema, "Hauwezi kufanya udanganyifu wa mwenendo."
  2. Mkristo asiye na lawama huishi maisha safi. "Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala uchafu, wala ya hila" (1 Wathesalonike 2:3). Mkazo wa Paulo hapa ni juu ya hisia za uchungu, tamaa. Anasema, "Hakuna kitu kilicho kichafu kilitoka kinywani mwangu. Mazungumzo yangu yalikuwa safi, yakitoka kwa moyo safi.” Mtu ambaye moyo wake umesafishwa hapaswi kusema utani mchafu, kufanya mazungumzo asioeleweka ya kingono au kuwa na macho yenye tamaa.
  3. Mkristo asiye na hatia iule hasemi uwongo, ambaye inamaanisha kuwa yeye sio mdanganyifu au mlaghai. Hakuna ajenda iliyofichika kwa mwamini aliemwaminifu na mwenye kuwa wazi. "Maana hatukuwa na maneno ya kufurahisha ... wala hatukutafuta utukufu kutoka kwa wanadamu, wala kwenu au kwa wengine" (1 Wathesalonike 2:5-6).

Kinachotofautisha kutokuwa na hatia, ni hamu kubwa ya kuheshimu jina la Yesu mbele ya watu wote. Mkristo kama huyo afadhali afe kuliko kufanya au kusema chochote ambacho kitaleta aibu kwa Bwana. Ingawa yeye sio mkamilifu, anafuata haki ya Kristo kwa imani.

Weka moyo wako kuwa wenye kutowa na hatia sasa - leo! Tamani hilo na kila kitu kilicho ndani yako, na hivi karibuni utagundua neema kubwa ya Mungu juu ya maisha yako. Maneno na vitendo vyako vitakuwa na athari nzuri kwa wengine unapojikuta unazingatia yote kabisa kwa Yesu.