ISIWE MUJINGA, YESU ANATAWALA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu anawalazimisha mataifa ya ulimwengu. Biblia inatuambia, "Atawala kwa uwezo wake milele; macho yake yanaangalia mataifa; waasi wasijitukuze nafisi zao" (Zaburi 66:7). "Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake unavitawala vitu vyote" (Zaburi 103:19).

Usiwe mujinga, nchi yetu haiongozwi na wa Republicani, Democrate au mamlaka yoyote ya kibinadamu. Haiongozwi na Wall Street au vyombo vingi vya biashara. Hakuna nguvu, ya kidunia au isiyo ya kawaida, inasimamia Amerika au taifa lingine lolote. Mungu peke yake yuko katika udhibiti. Anakaa kama Mfalme wa wafalme na Mfalme wa mabwana, anaongoza na kutawala juu ya viumbe vyote kutoka kiti cha enzi cha mbinguni.

Ninacheka wakati wowote nikisikia wanasiasa kujivunia nguvu za nchi yetu, jinsi tulivyojitambulisha wenyewe kama taifa la nguvu zaidi duniani. Hatukufanya chochote cha aina hiyo. Mataifa yote, wafalme, madikiteta na maraisi wa ulimwengu ni pigo tu la vumbi machoni pa Mungu. Bwana wetu anawaongoza wote, anashusha kiongozi mmoja na kuinua mwingine.

"Tazama, mataifa ni kama tone katika ndoo, huhesabiwa kuma mavumbi ndogo sana juu ya mizani; tazama, Yeye huvinyanyua visiwa kama kitu kidogo sana ... Mataifa yote mbele yake ni kama kitu, na wao huhesabiwa na Yeye kuwa chini ya bule na kutofaa" (Isaya 40:15,17).

Ikiwa Kristo anatawala kama mwenye mamlaka ma kuu juu ya ufalme wake, na sisi ni wasomi wake, basi maisha yetu yanapaswa kuongozwa na yeye. Ina maana gani, kwa kweli, kwa sisi kutawala na Yesu? Kwa mujibu wa kamusi, kutawala ina maana "kuongoza, kuelekeza, kudhibiti vitendo vyote na tabia vya wale walio chini ya mamlaka." Kwa kifupi, Yesu lazima aruhusiwe kudhibiti shughuli zote na tabia zetu. Anapaswa kuongoza na kuelekeza maisha yetu kila siku, ikiwa ni pamoja na mawazo yetu yote, neno na matendo.

Ruhusu Mfalme wako, Yesu, kutawala maisha yako kwa njia ya Neno lake, basi utabarikiwa na maisha yako yamejaa furaha yake.