HISIA TUPU NA ISIYO NA NGUVU

David Wilkerson (1931-2011)

Musa alikuwa na Mungu. Alipokuwa akiishi katika nyumba ya Farao, alikataa kuitwa mwana wa Farao: "Akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo" (Waebrania 11:25-26).

Hakuna usumbufu wa Mungu juu ya maisha ya Musa wakati alipokuwa Misri. Alijua kwamba aliitwa kuokoa Israeli; Kwa kweli, alidhani Waisraeli wangemtambua kuwa mkombozi wao wakati alimuua mtumishi wa mtumwa wa Misri. Stefano alitoa ushahidi juu ya hili: "[Akampiga huyo Misri]. Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokuvu kwa mkono wake" (Matendo 7:24-25).

Badala yake, Musa alilazimika kukimbia Misri kwa sababu ya matendo yake. Wakati alipokwenda aliuzwa kabisa kwa Mungu, ingawa hakujua kwamba alikuwa karibu kujificha upande mwengine jangwani kwa miaka arobaini.

Kipindi hiki cha jangwa katika maisha ya Musa kinawakilisha nini? Ni wakati ambao watumishi wengi walio na Mungu wanakabiliwa. Huenda ukawa mmoja wao, ukihisi kuwa umekwama katika mahali mbali ya uwezo wako. Musa alikuwa mtumishi kama huyo tu. Alikuwa na wito mkubwa juu ya maisha yake na aliota kwa kufanya kazi kubwa kwa ajili ya Mungu, Kwa kweli alikuwa kwenye ardhi ya maghalibi bila kuwa na muonekano wa baadaye.

Wakati Musa aliamini kuwa hakuwa sauti, na hakuna ujumbe, Mungu alikuwa anafanya kazi nyuma ya matukio. Siku moja alifanya kichaka kuwaka moto na kusema kutoka kwake, "Towa viatu vyako, Musa. Wewe uko juu ya ardhi takatifu! Sasa unakaribia kuona mambo makuu katika huduma yako kutoka kwangu."

Kichaka kilichowaka ulikuwa moto wa Roho Mtakatifu ikisonga mbele kupitia kitu kinachoonekana. Vivyo hivyo leo, Mungu anataka kujidhihirisha zaidi kwako ili wengine wawe karibu nawe watambue, "Mtu huyo amekuwa na Yesu." Unapomtafuta kwa nguvu mpya, utageuka kuwa mtu mpya, mwanamke mpya. Kama ilivyokuwa kwa Musa, siku zako bora bado ziko mbele.