FUNZA SIKIO LAKO KUSIKIA SAUTI YA KRISTO

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu bado anaongea na watu wake leo. Na anasema wazi kama alivyofanya katika Agano la Kale, au kwa mitume, au kwa kanisa la kwanza. Hata hivyo tunapaswa kutambua jambo moja: Mungu huchagua kusema tu kwa wale ambao wana masikio ya kusikia.

Marko anatuambia Kristo "aliwafundisha mambo mengi kwa mifano" (Marko 4:2). Katika kifungu hiki, Yesu anasema mfano wa mtu anayepanda mbegu katika shamba. Hata hivyo alipomaliza habari hiyo, umati wa watu ulikuwa unafadhaika na ukajiuliza, "Ni nani huyu mkulima anayeelezea? Na mbegu inawakilisha nini?"

Yesu hakuwaelezea hayo; Maana, Maandiko yanasema, "Yeye akawaambia," Yeye aliye na masikio ya kusikia, na asikie" (4:9). Wanafunzi wenyewe tu na wengine wachache walitaka majibu, hivyo wakaja kwa Yesu baadaye, wakimuuliza maana ya mfano huo: "Naye alipokuwa peke yake, wale walio karibu naye pamoja na wale kumi na wawili walimwuliza kuhusu mfano huyo" (4:10). Kisha Kristo alichukua muda wa kujibu mashwali yao yote (angalia 4:14-20).

Hebu angalia kile kinachotokea hapa. Yesu alikuwa amewapa ukweli wa ufunuo wa watu, neno lililonenwa moja kwa moja kutoka kinywa cha Mungu, lakini lilikuwa linawasumbua. Unaweza kujiuliza kwa nini Yesu hakuelezea kwa mfano wazi kabisa mwanzoni, lakini naamini alikuwa akisema, "Ikiwa unataka kuelewa Neno langu, utahitaji kunifuata ili upate jibu. Njoo kwangu kwa njaa ya ukweli ambayo itakuweka huru na nitakupa ufunuo wote unaohitaji."

Naweza kufikiria kwamba wakati watu wengi walipokuwa wakienda nyumbani, majirani zao waliwazunguka kwa kikundi, wakipenda kusikia yale Yesu aliyosema. "Tuambie yale yote muliyojifunza," walidai. Na wakati wao wangeweza kuwaelezea mifano, maneno yao yangekuwa yamekufa, bila ya kuishi, bila nguvu ya kubadilisha maisha. Ndio ambao walikaa nyuma, ambao walikaa mbele yake, ambao walipokea ufunuo wa Kristo wa kubadilisha maisha.

Je! Uko tayari kumngojea Kristo ili kupokea siri zake? Acha mambo ya raha zako ili ufanye chochote muhimu kinachokufundisha sikio lako kusikia sauti yake.