FARAJA ISIYO YA KAWAIDA

David Wilkerson (1931-2011)

"Na ahimidiwe ... Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote, ili nasi tuweze kuwafariji nawale walio katika dhiki ya namna yote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu" (2 Wakorintho 1:3-4). Kote duniani, watu wanapitia mateso na majaribio, na Bwana ameahidi kutufariji ndani ya hao. Ona kwamba hakuna kitu kinachosemwa hapa juu ya ukombozi kutoka kwenye vita; tunaambiwa tu kwamba Roho Mtakatifu anatupa faraja ya kuvumilia na kukaa imara katika jaribio letu.

Hii faraja, inayotolewa na Roho katikati ya shida zetu, si tu kuinua mzigo kwa kitambo. Sio  kupumuwa kutoka kwa faraja, kwa kutowa kelele ya mawazo ya kutisha au hofu. Badala yake, ni kitu ki sicho cha kawaida. Faraja hiyo ni huduma ya kipekee ya Roho Mtakatifu, inayotimizwa na imani tunapoamini kwa upendo wake kwetu.

Maandiko yanatuambia, "Utafariji watu wa Sayuni. Utakuwa na neno la uponyaji kwa wale walio kata tamaa na hofu" (angalia Isaya 61:2-3). Kwa kukabiliana na imani yetu, Roho wa Mungu huahidi kutengeneza kitu ndani yetu ambacho kitaleta faraja katika kila shida inayopokelewa na hali ya kutisha. Ataweka ndani yetu neno ambalo linaweza kuponya, faraja na kuhimiza wengine.

Roho alisema kupitia Isaya, "Nimeziona njia zake; nami nitamponya; Nitamwongoza pia, na kumrudishia faraja zake ... Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani" (Isaya 57:18-19). Hii ni mojawapo ya ahadi zenye kuhimiza zaidi katika Neno la Mungu. Bwana anasema atatuondolea roho ya hofu na kuingiza ndani yetu roho ya kawaida ya amani. Isaya anarudia neno "amani" hapa husisitiza kuwa ni amani ya daima.  Shikiria hili tu, Roho Mtakatifu ameahidi, "Nitaunda amani ndani yako."

Kama makukusanyiko ya mawingu yanayofanya hofu ulimwenguni, basi, unaweza kutembea kulingana na neno hili kutoka kwa Paulo: "Acha amani ya Mungu ihukumu moyoni mwenu" (Wakolosai 3:15). Amina!