FANYA HILI NA UTAISHI!

Gary Wilkerson

Watu wengi wanasumbuliwa kwa sababu hata ingawa wana ujuzi mkubwa juu ya Neno la Mungu, wana uzoefu mdogo wa maisha wanaoishi. Mungu anatutaka tuwe na mahusiyano ya kile tunachokijua na jinsi tunavyoishi.

Katika Agano la Kale na hata wakati wa Yesu, kujifunza sana Neno la Mungu ilikuwa sehemu muhimu ya maisha ya Kiyahudi. Mtoto wa Kiebrania alikuwa akianza shule akiwa na umri wa miaka sita na elimu yake ilizinduliwa na aya hii: "Sikiliza, Ee Israeli: Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja" (Kumbukumbu la Torati 6:4). Kisha, akiwa na miaka sita hadi tisa, alikuwa anajifunza Torati, vitabu vitano vya kwanza vya Biblia - Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati. Wanahistoria wengine wanatuambia kwamba watoto wenye ujuzi zaidi walikumbatia Torati nzima. Inashangaza!

"Onjeni na mwone ya kuwa Bwana yu mwema!" (Zaburi 34:8). Mwalimu kidini (Rabbi) alikuwa anataka kumwaga mda huo asali kwenye choko ya kuandika kwenye ubao wa darasani, kuingiza kidole chake katika asali, na kuaacha watoto kuonja. Kama asali ilifutwa kutoka kwenye ubao, urufu za somo zingeonekana. Nini njia nzuri ya kuanza elimu yako. Watoto walipokuwa wakiendelea kujifunza, walitengeneza tabia nzuri ya Kiyahudi ya kujadiliana - kujifunza jinsi ya kubishana.

Katika siku za Yesu "mwanasheria mmoja alisimama ili kumjaribu, akisema, 'Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?'" (Luka 10:25). Msomi mzuri wa kijana alikuwa na furaha kubwa ya kumshirikisha Bwana katika mjadala, kama Yesu alivyojibu: "Imeandikwa nini katika Sheria?" (10:26). Mvulana huyo akajibu, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote, na jirani yako umpende kama wewe mwenyewe" (10:27). Yesu alimwambia katika mstari wa 28, "Fanya hivi nawe utaishi" - kufanya wito kwa matendo!

Yesu kisha akasema mfano wa Msamaria Mwema, alitoa changamoto kwa mwanasheria huyo kijana, na aligeuzia ulimwengu wake chini sana. Alifafanua kwamba haikuwa ya kutosha tu kukariri au kuzungumza Neno, lakini lazima atende juu yake.

Wito wa Yesu huenda mbali zaidi ya kusikia tu na kukumbuka maneno yake; ni lazima tuyaweke katika matendo.