NJIA AMBAYO KIBURI KINAELEKEZA | World Challenge

NJIA AMBAYO KIBURI KINAELEKEZA

David Wilkerson (1931-2011)September 10, 2019

Kiburi kiko juu kabisa katika orodha ya vitu ambavyo Mungu huchukia. "Kwa yote yaliyoko ulimwenguni - tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha maisha – havitokani na Baba bali vyatokana na ulimwengu" (1 Yohana 2:16).

Wakristo wengi wangekubali kuwa hawajafika na kuna maeneo katika maisha yao ambayo yanahitaji uboreshaji, lakini wachache wangejiona kuwa wenye kiburi. Kiburi ni uhuru - unyenyekevu ni utegemezi. Kiburi ni kutokuwa na hamu ya kungojea Mungu atende kwa wakati wake na kwa njia Yake. Kiburi hukimbilia kuchukua mambo mikononi mwake wakati inaonekana Mungu hafanyi kazi haraka ya kutosha.

Mfano wa dhambi hii mbaya wa kutotii ni wa Sauli kule Giligali. Wakati Samweli alimtia mafuta Sauli kuwa mfalme, "Samweli aliwongea vizuri na Sauli kwenye juu ya yumba" (1 Samweli 9:25). Mjadala huu wa paa ulihusu vita kubwa ambavyo vilikuwa vinakuja na Samweli akamwagiza Sauli asichukue hatua hadi watu wote watakapokutana huko Giligali kumtafuta Bwana kwa maelekeo maalum. Hii ilikuwa ni kazi ya Mungu peke yake (ona 1 Samweli 10:8).

Samweli aliwakilisha sauti ya Mungu; chombo kupitia ambaye Mungu angewasilisha mipango Yake. Lakini Sauli alikosa uvumilivu na kuchukua mambo mikononi mwake. Mungu alikuwa akimjaribu na alishindwa kwa sababu ya kutovumilia - kiburi kisichosemwa!

Unyenyekevu ni tegemeo kamili kwa Mungu. Ni kumuamini Mungu kufanya jambo sahihi kwa wakati unaofaa katika njia sahihi. Na Yesu ametuachia ahadi tukufu ya kutuona kupitia siku za giza zijazo. Alisema, "Kwa sababu umelishika agizo langu kwa uvumilivu, mimi pia nitakulinda,  kutoka saa ya kujaribiwa ambayo itakuja juu ya ulimwengu wote, ili kujaribu wale wanaokaa duniani" (Ufunuo 3:10).

Download PDF